Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 7, 2010

THE GREAT NIKO NYUMBANI NILIKOZALIWA SHINYANGA KUMSALIMU BABA YANGU MZAZI NA NDUGU ZANGU.

Hapa nilikutana na msanii maarufu wa bongoflava NOORAH maeneo ya kwao ambapo ni karibu na home kwetu shinyanga wote tuko huku kusalimu wazazi wetu pembeni ni ndugu yangu Ayoub.

mimi na shemeji yangu saloon kwake shinyanga mjini.

hapa niko na baba yangu mzazi baba the great Mzee Charles Meshack Kusekwa Kanumba tukigonga vizuri lugha ya kisukuma.

mda wote nyumbani kumezungukwa na watu hasahasa watoto wengi kila mara wanataka kuongea na The great mtoto wa nyumbani kokaya.


Ilinibidi niwaridhishe kwa kuongea nao.

hali ilikua hivi mda wote hadi usiku


Nikajaribu kupita mlango wa uani-nyuma ili nikakate mitaa na Noorah bado napo walikuepo huko.hapa wanataka kushikana mikono live na The great.


Wengine walinisubiri katika gari nililokua natumia ili nipige nao story nami nilifanya hivyo.Nilitembelea Mwadui nikapewa na flana yenye maandishi yanayomaanisha Wadau wa kazi za injili mwadui(WKZI-MWADUI)kushoto ni joshua ambae kipindi nasoma mwadui seminary sec school niliimbia kwaya yake na nilikua nikipiga kinanda,kulia ni Ipyana Mwakatenya yeye alikua ni mfadhili na kaka yetu mkubwa katika kwaya yetu ya shule wakati huo mimi nilikua choir master wa shule na UKWATA.

Nilitembelea hospitali ya mwadui kuona wagonjwa lakini pia kama kumbukumbu kwangu maana hospitali hii niliwai kutibiwa typhod wakati nipo boarding school.

kushoto ni Mrs Ipyana Mwakatenya,wauguzi mbalimbali na The GP.

Pia nilitembelea shule yangu niliyoanzia form one ya Mwadui seminary secondary school kuwatia moyo wanafunzi.

wakati wa picha ndio kama unavyoona wote walitaka kuwa karibu na mimi

Niliwapa mawaidha mazuri kwamba hata Biblia takatifu imesema mshikeni sana Elimu msiache iende zake,kile apandacho mtu ndicho avunacho.


Wengi wanafunzi walishangaa walipoambiwa kuwa niliwai kusoma hapo na nilikua nikiigiza na kuimba katika matukio maalum ya shule wakati huo sikujua kama ipo siku nitakua hivi nilivyo sasa na kuna vipindi nilivyovianzisha hapo shuleni hadi leo vijana wanaviendeleza bila kujua muasisi ni nani mfano kipindi cha kusali na kuabudu kila siku jioni kwa wanafunzi wa boarding.

3 comments:

Anonymous said...

Kanumba wewe Mungu anakupenda sana na unaonekana kutokuwa mbali sana na neno la Mungu.Sasa basi jitahidi sana na uwe muangalifu usije ukamaliza vibaya ,,kwasababu umeokoka ukiwa bado mdogo na kwasasa nikama unathamini sana mali.Tunakuombea sana umuludie mungu.

Anonymous said...

Kanumba kaka umevaa cheni ya mpinga Kristo nafikiri bila kujijua,nenda ==kagoogle signs za mpinga kristo na alama ya iyo cheni ipo

Anonymous said...

Du, dingi yako anajua kulenga, mwanagu sura copyright, mnafanana mpaka vimvuli, samahani kama nimeku offend.