Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 21, 2010

KANUMBA THE GREAT FILM bado tupo mzigoni tukipika kitu kipya jina bado kapuni ila shughuli yake ni pevu.

Aunty Ezeckiel na Kijana wangu Suma wakionesha uwezo wao katika scene ya mapenzi kitandani.kama ilivyo kawaida yangu mbali na kuweka mastaa katika movie lakini pia huwa naweka na vipaji vipya vinavyochipukia ili nao wapate nafasi ya kuonesha uwezo wao kama unavyoona hapo juu.

Baada ya kumaliza scene Gwantwa aliamua kupozi kwa picha kidogo huku kijana Suma akichekelea kwa kumaliza scene yake vizuri.


Aunty Gwantwa na Patcho Mwamba wakipokea maelekezo toka kwa director kabla ya kuanza kurekodi


Kazi imeshaanza Aunty na Patcho.

Katika movie hii Patcho kaonesha kiwango cha juu sana huwezi amini kama ni mkongoman tena mwanamziki wa bendi maarufu jijini ya FM ACADEMIA.The great kazini mbele ya kamera.

Huwa sina masihara kabisa ninapokuwa mbele ya kamera ninashukuru sana Mungu maana kila filamu huwa naonesha maajabu na hii itakua funga kazi

Patcho na Aunty walijisahau wakalala kweli nilipowagusa na fimbo yangu walishtuka kwa kelele sana ikabaki vicheko kama unavyoona hapa hivyo ikabidi turudie.


Hapa wamelala kabisa wamejisahau hii utokea mara kadhaa wakati setting za taa na kamera zinapochukua mda mrefu wakati wasanii wako tayari hupitiwa na usingizi.

Hapa nikikagua setting ya kila kitu wakati wasanii wangu wanakoroma.


Picha ya juu na chini nikiwapa maelekezo juu ya nini wafanye katika scene hiyo nao husikiliza kwa makini sana.Ni picha tu jamani

Kutokana na makamuzi anayoyafanya Aunty katika movie hii kwa sasa pindi anapomaliza kila scene hata crew yangu nayo hutaka kupiga nae picha maana humuona ni mpya tena.

Lusubiro akipiga shot ya kiatu namkumbuka director wangu wa kwanza katika tamthilia anaitwa Chrissant Mhenga hizi alikua akiziita shot za upendeleo kipindi hicho tukiwa kaole sanaa group.

Nikishauriana jambo na cameraman wangu Lusubiro.

Wakati fulani huwa inabidi nitizame katika screen ya camera ili nione kama monitor yangu inanipa picha sawa na ya kwenye camera maana kama monitor setting yake si nzuri basi huweza kukudanganya na kukupa picha usizozitaka lakini pia kuwa na uhakika na angle ya kamera kama hujacross angle.

Nikitoa maelekezo kwa crew jinsi scene tunayoelekea kushoot ilivyo ili tujue kamera na taa vikae sehemu gani.


Kazi ikiendelea

Jicho langu la kushoto limekua jekundu baada ya lenzi ya macho niliyokua nikitumia kudondoka chini na aliyeniweka akuiosha vizuri katika maji yake hivyo ikaingia na vumbi na kusababisha jicho langu kuniwasha sana hivyo nikaamua kushoot bila lenzi lakini kazi inakwenda vizuri...ni mambo ya kawaida mkiwa shooting.

Gwantwa akaona bora asiache mbachao kwa msala upitao muone alivyofanya macho yake na ulimi.

Kutokana na wingi wa taa ukijumulisha na hali ya hewa ya DAR basi joto huwa kali sana hivyo mtu wa make up huwa busy sana kuakikisha kila unapotoka jasho kuja kuliondoa maana huwa hatuwezi kuwasha air condition au feni maana hutoa kelele ambazo hualibu audio ya movie,Maya akinisaidia yeye ndie make up artist wangu na Production manager.

5 comments:

Anonymous said...

Ezekiel umependeza, I wish ingekuwa siku yako ya harusi kweli.
Mungu atakupa tulia na ongeza juhudi katika kazi.


disminder.

Anonymous said...

inawezekana yakawa maisha ya kweli ya aut ezekieli katika young milioneal

Anonymous said...

Aunty looks veeeeeery cute as if its a true wedding of herz. kaza buty mamie u r a really movie star.

Anonymous said...

Aunty looks veeeeeery cute as if its a true wedding of herz. kaza buty mamie u r a really movie star.

Anonymous said...

Aunty looks veeeeeery cute as if its a true wedding of herz. kaza buty mamie u r a really movie star.