Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Mar 8, 2010

SIKU ILIYOFUATA NILIELEKEA KIJIJINI ALIKOZALIWA MAMA YANGU MZAZI KUWASALIMIA BABU NA BIBI UPANDE WA MAMA YANGU PIA KUJUMUIKA PAMOJA KATIKA HAFLA YAO.

Nikishuka katika ndege ndogo kuelekea katika kijiji.

Sijui nielekee huku au kule?

maskini babu yangu aliponiona tu alilia sana kwa furaha maana mara ya mwisho tumeonana nikiwa darasa la nne na alinipenda sana,alisema mjukuu wangu nilijua mpaka nitakufa bila ya kukuona tena,mbali na uzee babu yangu anasumbuliwa sana na kisukari.

Nilimbembeleza anyamaze maana nimeshafika nae akatulia ndipo tukapata picha ya pamoja,kwa ufupi miaka ya sabini na themanini babu yangu huyu upande wa mama aliwai kuwa daktari mkuu mkoa wa mwanza na tabora kabla ya kustaafu na aliyekua Raisi wa awamu ya pili Tanzania Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi alimpatia cheti maalum cha kutoa matibabu popote pale atakapokuepo katika kustaafu kwake kazi ambayo ameiacha mwaka juzi baada ya uzee na ugonjwa wa kisukari kumsumbua sana,pole sana babu.

Kulifanyika ibada maalum ya kuadhimisha miaka58 ya ndoa ya babu na bibi yangu walialikwa watu kadhaa na kwakua tuko katika mfungo wa kuelekea pasaka watu walikaa chini ili kushiriki pamoja mateso ya Mwokozi YESU KRISTO.

Babu na bibi yangu walizaa watoto sita wote wamefariki amebaki mama yangu tu hivyo ilinibidi niende katika makaburi ambayo yako shambani mwao kuweka mashada na mishumaa kwani katika kipindi cha hiyo misiba yote sikuwai kufika.

Nilishindwa kuvumilia nilipofika katika kaburi la marehemu mjomba wangu(Robin)mbali ya kuwa mjomba wangu lakini alikua ni rafiki yangu,tulikua karibu sana.machozi yalinitoka.aliyekaa chini ni bibi yangu akinionesha kaburi moja baada ya lingine na kunitajia hapa tulimzika flani na pale flani yeye alikaa chini akilia.

Hapa alizikwa marehemu mama mdogo wangu miaka kadhaa iliyopita hivyo nikiendelea na zoezi hilo makaburi yamepangana hapo shambani.

Aliyembele yangu ni mama yangu mzazi akinisaidia kunipa mashada na mishumaa na ndie aliyebaki katika uzao wa bibi na babu yangu baada ya wote kufariki.

Mchungaji akiongoza sala huku bibi akilia,mimi na mama yangu tukisikiliza kwa makini

Nikimuongoza bibi kutoka shambani baada ya zoezi zima kumalizika.

Miaka 58 ya ndoa yao babu na bibi yangu niliwapa zawadi yao kama mjukuu wao nao walinibariki sana.

watu wa rangi mbalimbali walikuepo kuwapongeza babu na bibi yangu.

17 comments:

Tibella said...

Thats nice man. Appreciate.

Anonymous said...

hongera kaka yangu kwa kuwatembelea wazee twawatakia maisha mema ya furaha na amani.na mgonjwa baba yetu na twampa pole sana.
dada s.
dk

Anonymous said...

Mzee wajengeeni wazazi kuliko kutanua Dar. Nakufagilia sana kutembelea nyumbani lakini jenga bwana hasa hapo kwa babu.

Anonymous said...

kanumba nakupongeza sana hata kwa wewe unayekumbuka nyumbani kwenu na kujivunia maisha ya kwenu mana kuna wengi hawaendi kwao na wala hawataki watu wapajue kwao wanaona aibu kuwaonyesha hata babu bibi zao.,

ushauri ni kwamba muda umefika wa wewe kupeleka mke kwenu apate baraka za babu na bibi

peleka hata bibi harusi mtarajiwa,
usipeleke vicheche!!


judith

Mama Kelvin said...

Hongera sana the great ni watu wachache sana wanaopata umaarufu kurudi nyumbani (kijijini) kujumuika na familiya katika vitu muhimu kama hivyo. umebarikiwa kijana

Anonymous said...

Jengea makaburi hayo Kanumba naamini uko katika position hiyo na Mungu atakubariki.

Anonymous said...

kwaninin ulingojea miaka yote hiyo kwenda...cuz najua haiwezekani ukaishi darsa la nne mpaka leo hii bila hata kuwafikiria wala kufikiria kwenda...???

Mary said...

Safi sana kaka,ni jambo la kheri kuwakumbuka waliotutangulia. Pole sana kwa yote,ni maisha ambayo kila mmoja wetu atayapitia,pole zangu pia kwa bibi na babu kwa kupoteza watoto wote na kubaki na mama pekee. Mungu akutangulie katika yote ufanyayo!

kokusima said...

Umeniliza pia kakangu, nimeyakumbuka makaburi ya wazazi wangu na ndugu zangu yalivyojaa shambani kwa bibi Karagwe. Umefanya vizuri kuwatembelea wazee wako na nivyema uwe unaenda mara kwa mara ili wazidi kukubariki, manake tangu uwe darasa la nne nazani itakuwa vya 96 km si 97 manake miaka yako ka yangu tu. Mungu awarehemu marehemu. amen.

Mariam said...

kwakweli i have nothning against u kanumba but i think the quality of ur pictures look, for the lack of better words,they look cheap.

Plz improve it,sijui ni kamera yako au ni nini ila picha zako sio nzuri.

Mariam.

Anonymous said...

jamani kanumba naomba ufanye hima ujengee hayo makaburi ya aunt na uncle zako wapumzike pasafi

Anonymous said...

uuuwiiiiiiiii kanumba jenga kwenu jamani mwemwe!! unakaa kujiita the great wakati mmh!ndio maana nawapenda wachagga wanapenda kwao na wamejenga kwao.acha ujinga dogo endeleza kwenu

Anonymous said...

we mwanaume kumbe una kwenu loh tena una familia lakini sidhani hata kama unafanya maendeleo huko kwenu hiyo nyumba loh halafu wewe ukizingatia unaingiza senti jamani unashindwa kujenga nyumba nzuri huko kwa bibi loh mshinyanga wewe ila unaonesha wewe una mkono mfupi sana kijana!!!!!!hongera kazi nzuri ilaa fanya maendeleo kijijini kwenu na mtu ukikulia kijijini siku ukienda wanaona kama wameona msanii kutoka majuu vile hahahahahahahah aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

hauoni hata aibu kusema toka darasa la nne haujarudi kwenu, eti shangazi zako na wajomba wanakufa lakini hata kuzika hauendi ilihali unaishi hapo tu dar es salaam, je na wanaoishi ulaya wasemeje?

Ester Ulaya said...

Maskini babu anamlilia mjukuu, uwe unaenda marakwa mara, mfanyie hata surprise ya Kumshoot kwenye movie zako?

Machuma said...

Big up kanumba, kwa kweli umefanya vizuri sana kuwatembelea babu na bibi yako kule kijijini, umeonyesha mfano mzuri sana keep it up, huo uwe mwanzo na sio mwisho lakini pia liwe somo kwa macerebrity wengine Bongo na mafanikio yataongezeka maradufu.

Anonymous said...

hivi kweli toka darasa la4 mpaka sasa ndio unamuona babu yako' alafu mnamsifia ujinga? hiyo ndio kawaida yawatu waliozaliwa mikoani wakifika mjini basi