Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Sep 16, 2010

THE GREAT AMTEMBELEA MZEE KIPARA KIGAMBONI

The great nimeamua kumtembelea mzee wetu,msanii mkongwe wa maigizo na mwasisi wa kundi la KAOLE SANAA GROUP kundi ambalo mastaa wengi wa movie tulianzia hapo na tumetokea hapo.Safari yangu ilikuwa mida ya jioni nilipokewa na mzee mwenyewe MZEE KIPARA.Kwa kifupi mnamo mwanzoni mwa mwaka 2001 The great nilijiunga na kundi la KAOLE na MZEE KIPARA ndiye aliyenipokea na kuniwezesha kujiunga na kundi hilo akiwa sambamba na MAREHEMU MZEE PWAGU,Tuliishi vizuri sana hadi kufikia hatua ya kuondoka kundini hapo na kuanza kucheza filamu ambazo zimenifikisha hapa nilipo nikiwa na kampuni yangu.Kundi la KAOLE lilianza kupoteza umaarufu wake mara baada ya mastaa waliokuwa wakicheza tamthilia humo kujiondoa kutokana na masilahi na uongozi kuyumba hadi wazee wetu kuondolewa katika nafasi zao za uongozi na hata sisi wengine kuondoka kundini humo.Mzee KIPARA anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu ambapo kwa mujibu wake kanambia hospitali kadhaa alizoenda hawaoni tatizo japo miguu inamuuma.Naombeni tuzidi kumuombea mzee wetu na kumsaidia kwa chochote tulichonacho ili hali yake irudi kama zamani. Tukiongea machache na Mzee Kipara chumbani kwake

Nikijaribu kushika miguu yake katika sehemu anazosikia maumivu

Nikiwa nimeshika baadhi ya dawa za asili anazotumia,na nikimuuliza jinsi zinavyomsaidia

Akiniambia jinsi tatizo la kifedha linavyomsibu

Akizidi kuniambia jinsi anavyoteseka na miguu

Nikimpatia kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya matibabu

Mzee kipara akinishukuru kwa kuja kumuona nami nikamuahidi ntakua nakuja mara kwa mara kumuona na kumpigia simu kila wakati kujua anaendelea vipi lakini pia nimemuahidi kuwa ntaongea na madaktari bingwa katika hospitali kubwa ili kuona kama suluhisho laweza patikana hivyo nikamwambia mda wowote awe tayari iwapo nitafanikisha nitamfata kumpeleka ili apate tiba sawia

Akinisindikiza nje wakati wa kuondoka

Nikizidi kumtia moyo mzee wetu

Kama kawaida watoto kwangu ndio mashabiki wangu namba moja waliponiona hawakusita kunikimbilia

Basi hapo kila mtoto na swali lake,wengine wakiuliza uncle jj jenifa yuko wapi??

Ilibidi niwe makini kuondoa gari yangu ili nisije kuwagonga maana hawakutaka niondoke walizingira gari yangu

45 comments:

Anonymous said...

hama kwa hakika unastahili pongezi Kanumba,nimekuwa msomaji mzuri wa bog yako nikuvutiwa na ujasiliamali ambao unaufanya na kutengeneza ajira kwa vijana na wazee,

hii post imenivutia sana na ile ambayo ulienda kumsalimia babu yako nadhani ilikuwa mwanza au shinyanga,

endelea na moyo huo kaka

Anonymous said...

na kweli mashabiki wako maana mmemeshisha mpaka viatu kaka na hao watoto..

Anonymous said...

kaka mungu azidi kukuzidishia yaani hio tour ya kwa mzee kipara ni babkubwa.kitendo tu cha ww kwenda ni dawa nahisi hata maumivu ya miguu kwa siku hiyo yalipungua.kweli umeonyesha ukomavu wako kisanaa.na macelebrity wengine wa sanaa waige mfano wako.yaani mie binafsi nimejisikia raha sana sasa sijui mzee kipara mwenyewe.god bless u.

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu akujalie na akuongezee pale ulipotoa akupe mara dufu Inshallah. Uendelee kuwa na moyo wa imani leo mpaka kesho akhera.

Anonymous said...

Kanumba, umelelewa katika mikono salama yaani umefanya kitu kizuri sana maana mpo wasanii wengi mliofaidika na mzee huyu lakini hata hawakumbuki wanalewa tu sifa za kuitwa mastaa You did good things na mungu atakuzidishia

Deliwe

Anonymous said...

safi sana Kanumba kwa kwenda kumuangalia hy mzee wenu na kumsaidia na bado kuendelea kuahidi kumsaidia. nawaomba wasanii wengine wajitokeze pia katika kumsaidia mzee Kipara.

Furaha
DSM

Anonymous said...

ohh God bless you Kanumba,hadi machozi yamenitoka kwa hisia,maana na mimi uwa napenda sana kusaidia wahitaji

Anonymous said...

Mungu akubariki brother,endelea hivyo.napenda sana filam zako lakini na ishi abroad.sijui nitazipata je?
take care

Anonymous said...

at least umemkumbuka. Mungu na akuzidishie pale ulipotoa paongezeke..

Anonymous said...

God bless u 2 the maximum, u know ni watu wachache sana wanaokumbuka kuwasaidia wazee ambao hawana msaada,bro for this God wil make a way in your life!Zuwena

Mama twins said...

Hongera sana Uncle JJ, kama wanavyopenda wanangu kukuita siku hizi. Mungu akuzidishie uendelee na moyo huohuo wa kumsaidia mzee Kipara labda kupitia kwako, Mungu anaweza akairudisha afya yake kama hapo zamani. Ubarikiwe saana Uncle JJ!

BQ said...

aisee big up sana Kanumba hapo kweli umefanya jambo la maana sana maana huyo mzee wengi wamemsahau wamesahau kuwa huyo ndo kawatoa kupitia kaole,Mungu akubariki na kuzidishie hapo ulipopunguza.

Anonymous said...

Katika watu wananiuma ni huyo mzee jamani nilimuona Kiria aklimtoa kwenye Bongo Movies machozi yalinitokakanumba Mungu akuzidishie maradufu tafadhali msaidie tena ikiwezekana haraka na Mungu atakubariki

Anonymous said...

Hongera sana kanumba. Nimefurahi sana kwa huo moyo wako ulioonyesha kwa mzee wenu. na baba yenu wa sanaa. Lakini tafadhali bro hizo ahadi ulizomwahidi make sure unazitimiza maana umeahidi. Usijeukapuuzia jitahidi umsaidie kadri uwezavyo. Ni hayo tu.

Emmy[Mwanza]

Anonymous said...

ur great kwa kweli nimefurahishwa na kitendo hichoo sana big up!

ila kanumba unaonaje kama wasanii mkajichangisha au mkafanya lolote la kumsaidia huyoo mzee mana ameanza kulala mika siku nyingii hebu jitahidinii jamanii au mnataka kwenda kutoa rambirambii eeenh plzzz, fanya hata event yoyote si kwenda peke yakoo jiandaenii wasanii kadhaa mbona mnaweza jaamanii plz simamia hilo
wanguu anatia huruma huyo mzee anaonyesha hata chakula anachopata hafifuu mumkusanyie hata vyakula, mi nimeguswa kibinadamuu ila u know kibinadamu inasikitisha natamani nifanye kitu flanii kama mwanajamii bt nashindwaa ok kaka kazi njema
na mafanikio mema

mwanaid,

Juma said...

Kanumba mungu akubaliki ,kitendo cakusaidia watu kama hao hata Mungu anaweka vema,,ingawa sisi wanadamu kuna maovu tunayoyatenda lakini kazi kama hii lazima inalekuletea balaka nyingi,,na ndio maana kazi zako zitaenderea kuwa juu ya wengine.

Anonymous said...

that isvery gud the GREAT yani Mungu atakubariki kwa hilo ulilofanya! kumtembelea huyo mzee ni baraka kubwa sana.

Mzee wa Changamoto said...

Great stuff mankind.
Hongera kwa kumjali na kurejesha fadhila. Umekumbuka kuwa alichofanya mzee huyu ni KUWEKEZA kwenye maisha yenu na sasa kile alichowapa ni zaidi ya pesa taslimu ambazo alitoa wakati huo.
Hakuwapa mlo, bali kawapa jembe na shamba na sasa mnavuna
Shukrani kwa kutambua hili na naomba taswira kutumia kwenye post yangu
Blessings

Anonymous said...

Hi, Ni vizuri sana kanumba m.mungu akutie wepesi ili ufanikishe ahadi yako ya kumtafutia daktari ila naona hapo wewe na mashabiki wako mlimechisha kweli hawo nimashabiki ile mbaya watatu wote kijani safi sana hongera sana kaka.

HAPPY said...

kwanza nakupongeza kumtembelea huyo mzee.pili mimi ni mdau namba moja wa filamu zako kila ikitoka lazima ninunue tena orginal lakini jmosi nilinunua filamu ya more than pain kwa kweli kanumba siku yangu ilikuwa nzuri sana wakati nikitaza ile movie nimecheka kila nikikumbuka nacheka na hasa ulipoenda kwa baba yake lisa kujieleza.halafu the way unaporudi na kumwelezea lisa that you have good news.kanumba your a fire real umedhamilia na kipaji unacho my bro.HONGERA SANA KWA KAZI YA MORE THAN PAIN

Anonymous said...

the great Mungu azidi kukuongoza katika hili mawazo binafsi tu kama unaweza nafikiri ni vizuri kupitisha harambeepia tukipata ni njia gani tunaweza kufikisha michango yetu kupatafuta nyumbani kwake ni ngumu tunaomba mawasiliano tuweze kutoa michango yetu.

MwanaRuganzu said...

Ndio kijana!Umefanya jambo la busara sana.Kwani hao ndio wakunga wetu.Ni vizuri kukumbuka tulipotoka.Hizo ni baraka pia.Nawaomba wasanii wengine waige mfano wako!!

BOB T - KIGALI

mfalme edo said...

kaka umetumia busara sana kumtembelea huyu mzee bwana na ujitaidi kama ulivyosema apate matibabu I wish ningeweza kusaidia lakni uwezo mdogo

Milly said...

Huo ndo uzalendo ambao watanzania wengi tunaitajika kuwa tunafnya.Big up Kanumba kwa hilo imenifanya nianze kuwa mmoja wa washabiki wako.

Mungu akuwezeshe zidi ya hapo.

Anonymous said...

Hahahaah Kanumba nimecheka nilipoona mmevaaa viatu sare sare na mashabiki wako yaani nimejikuta nacheka mwenyewe sijui walijuwa jamaa kavaa green shoes nasi tuvae hihiii safi saaana, Lakini kitu kimoja nakuomba next time when u give somebody/one things like money pleeaaaseeee dont show the pic to the public ungechukuwa tu picha km kumbukumbu yako lkn usiiitoe km ulivyofanya nimeona kwenye Gp pia, hapo malipo kwa Mungu ni asilimia 1-5 laiti km unsingeweka picha basi ni I'm sure ni 100% ni ushauri tuuu usikuumize saaana. keep going

Mdau kwa Obama USAgara a.k.a Mchafukoge or Mama NJ

Anonymous said...

kanumba umefanya kitu kizuri sana na huo ni mfano wa kuigwa na wasanii wengine, mungu akubariki na akuzidishie

MloMmoja said...

to be honest sikuona sababu za Kanumba kumkabidhi fedha uku akimpiga picha Mzee Kipara, angeonesha tu kwamba amemtembelea. Nakupa hongera japo nimetilia shaka lengo lako la kwenda kumtembelea,unaonesha una roho dhaifu kaka,umempiga picha ili siku akilalamika utoe ushahidi, coz mlipokutana pale leaderz alisema amewaonesha njia lkn mmemtupa, umemdhalilisha uyu mzee...kuna misaada ahiitaji media hype,tuweni wastaarabu.

Anonymous said...

Hongera sana Kanumba kwa kumtembelea huyo mzee endelea na moyo huohuo mungu atakubariki pia napenda sana unavyo igiza namba moja Tanzania nzima unatisha kama Obama

Anonymous said...

Hongera sana Kanumba kumtembelea huyo Mzee wetu pia nakupungeza kazi zako uko juu kama Obama

dsindano.blogspot.com said...

Vizuri sana kaka,kuwa na moyo huo daima na Mwenyezi Mungu akubariki katika kazi zako.

moi said...

ebana mumgu akuzidishie kwa kukumbuka fadhila kumtembelea mzee wako kipara uwe na moyo huo huo kaka

Anonymous said...

yap kanumba big up sana kukumbuka mzee wako wa zamani kwa kuwa wengi wansahu walipototka yani hapo utajiona una amani na utafanya kazi zako kwa kubarikiwa huwezi jua mungu atakupa baraka gani kupitita mzee huyo ubarikiwe sana.(Lily)

Anonymous said...

Umefanya jambo la busara Ndugu ila hiyo ya kujipiga picha wakati unampa hela sijaipenda kwa kweli.next time si mpaka iandikwe kwenye gazeti ndio ufanye wema kaka,butyou did a good thing na kila la kheri.ni hayo tu

Anonymous said...

Hongera sana

Anonymous said...

Mwana sifagilii kabisa movie zako ila kuna matukio mawili umeyafanya M/Mungu atakulipia moja lile la kwenda kwenu Shinyanga na hili la kutambua umuhimu wa mtu aliekuonyesha njia na kwenda kumuona kipindi muafaka maana kuuguza ndio muhimu sio siku kafa mnaenda na mahela magharama ya chakula wakati anaumwa hakuna aliekwenda kumuuguza. SASA WW SIO THE GREAT WW NDIO THE GREATEST MWENZIO YY ANAJIPAKAZIA TU. HONGERA SANA KIJANA

msafir said...

hii safi sana mkuu umeonyesha moyo wa kipekee sana kumkumbuka huyu mzee,na nadhani utabarikiwa zaidi kumpeleka hospitali.agha khan ni wataalam sana na mambo ya kutibu miguu kawaone watamsaidia.

Anonymous said...

good job K!

Anonymous said...

Good job Mr K!

Anonymous said...

Good job Mr K!

seychelela msamba said...

what u did kanumba is remarkable umeonesha ni kiasi gani unajali walio changia ufike hapo ulipo what i advise u is that u need to remember ur promise and keep on helping him and ukiweza mpe featuring kwenye movies zako utakua umemsaidia siyo tu kifedha bali utarudisha heshima yake kwenye ramani ya film industries and plz try to organise ur selves as artist muanzshe foundation yenu itakayo wasaidia mkifika finaly{uzeeni

seychelela msamba said...

what u did kanumba is remarkable umeonesha ni kiasi gani unajali walio changia ufike hapo ulipo what i advise u is that u need to remember ur promise and keep on helping him and ukiweza mpe featuring kwenye movies zako utakua umemsaidia siyo tu kifedha bali utarudisha heshima yake kwenye ramani ya film industries and plz try to organise ur selves as artist muanzshe foundation yenu itakayo wasaidia mkifika finaly{uzeeni

Anonymous said...

kaka hongera sanaaaaaaaaaaaaaa kiukweli una moyo wa kipekee coz wasanii wenga ss hv hawakumbuki walipotokea, ongeza juhudi tu kaka Mungu yupo pamoja na ww

Anonymous said...

ndio maana original comedy wamekuigiza.... yaani unapeleka msaada na kumpiga picha? hata mungu hapendezwi na hiyo sadaka yako.mi nauita ushamba kwani ulishindwa kumpa kimya kimya?

Anonymous said...

Hongera Kanumba kwa ulichofanya, wengi wanaweza kusema au kujiuliza ni vipi unafanikiwa katika maisha yako, ila napenda kukufahamisha kuwa kwa vile utoavyo na kukumbuka waliokusaidia kufikia lengo lako ndipo unapozidi kutakaswa na kuweza kwenda mbali zaidi kimaisha. Naamini kabisa Mzee Kipara aliomba au kusema dua kimya kimya ya kukutakiwa mema na fanaka tele maishani mwako. Mungu akubariki na akuzidishie Hekima na akili ya kukumbuka waliokusaidia.

Anonymous said...

Hongera Kanumba kwa ulichofanya, wengi wanaweza kusema au kujiuliza ni vipi unafanikiwa katika maisha yako, ila napenda kukufahamisha kuwa kwa vile utoavyo na kukumbuka waliokusaidia kufikia lengo lako ndipo unapozidi kutakaswa na kuweza kwenda mbali zaidi kimaisha. Naamini kabisa Mzee Kipara aliomba au kusema dua kimya kimya ya kukutakiwa mema na fanaka tele maishani mwako. Mungu akubariki na akuzidishie Hekima na akili ya kukumbuka waliokusaidia.