Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Sep 7, 2010

KANUMBA THE GREAT FILM MZIGONI.

The great nimeanza kuandaa kazi yangu mpya iitwayo UNCLE JJ nikiwa na wanangu wale wale waliokamua vizuri katika THIS IS IT safari hii tuko bush ni full vituko na vunja mbavu,bado nasimama katika msimamo wangu wa kuinua vipaji vya watoto wadogo kabisa nadhani hata ninyi ni shahidi wa hilo,uncle jj,jenifa na patriq twakamua humu chini ya kampuni yangu ya KANUMBA THE GREAT FILM,nikitumia vifaa vyangu mwenyewe nilivyonunua yaani kuanzia camera hadi vifaa vya editing ni vyangu tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ikinilazimu kukodi,hakika najivunia hili kwani kwa sasa nafanya kazi bila presha na namshukuru Mungu kwa hatua hii kuanzia kuwa na kampuni yangu mwenyewe,ofisi yangu lakini kubwa zaidi ni kumiliki vifaa vyangu mwenyewe vya production kuanzia shooting hadi editing Uncle jj na Jenifa ktk makamuzi

Tukishangaa kitu katika scene

Patriq na Jenifa yaani hapa wanangu wamekamua kisawasawa mpaka nimejivunia kuwa nao,nikajivunia kuwaleta katika ulimwengu wa sanaa ya filamu maana ni moto wa kuotea mbali ni zaidi ya This is it

Kama umetizama This is it lazima utajua moto wa huyu Jenifa sasa hapa kituko alichokifanya me si sisemi mtaona tu jamani ndo napika mambo

Patriq na watoto wenzie

Toka niwatambulishe katika ulimwengu wa filamu Jenifa na Patriq kupitia filamu yangu ya This is it wamekuwa gumzo mtaani hata kwa watoto wenzao kila wanapopita inawalazimu kupiga picha na wenzao jambo ambalo nao kwa sasa wanaanza kuzooea hawakatai maana nimeshawafundisha nini maana ya kuwa Star,mbali na hayo nawasimamia shuleni kuhakikisha wanasoma vizuri na kupata elimu bora hii ni kutokana na uwezo wao katika sanaa

Asilimia kubwa Jenifa ndie anayepata usumbufu mkubwa sana kuliko mwenzie lakini bado anaonesha upendo kwa watoto wenzake na kuwajali kama hivi unavyoona

Jenifa kazini mbele ya camera

The great na Cameraman wangu Farid Uwezo ambae ndio mara ya kwanza nafanya nae kazi,kila mara anasema kwa mda mrefu sana nilitamani kufanya kazi na wewe na leo ndoto yangu imetimia tena nikitumia camera yako ya kiwango cha juu,Jamani hiyo ndio camera yangu ninayomiliki kwa sasa chini ya kampuni yangu ni kifaa ninachojivunia kukinunua maana uwezo wake ni mkubwa mno katika picha pia ni producer wachache sana nchini wanaotumia na kumiliki camera kama hii,ni SONY DSR 390

14 comments:

Albert said...

Hongera sana Bwana Kanumba kwa hatua nzuri ulioifikia ya kutengeneza filamu, tuna uhakika kwamba kwa sasa utafanya vizuri zaidi ya hapo mwanzoni kwa kuwa kampuni yako ina kila kitu.
Na sisi kama mashabiki wako tuko ready kwa kukipokea kile unachotupatia. Kazi zako ni nzuri sana tunazi appreciate, na kama sio roho mbaya tu, lazima kila mtu aani sapoti kwa hili.
Congratulations Bro......!!!??!
Albert
Western Australia.

Lulu said...

Ahsante Kanumba kukuza vipaji vya watoto, ila waache wafaidi utoto wao msiwafanye kama Diana na Eliza maana watoto wamekuwa wakubwa ghafla.

merido said...

kaka kanumba hv ndo nilikuwa natakayaani blog inachangamka na matukio endelea kutujuza

kashubi said...

Kanumba hongera sana hasa kwa kuweza kumiliki vitendea kazi, kwa kweli hii ni hatua kubwa ya maendeleo umeifanya, mwenyezi Mungu aendelee kukubariki na kubariki kazi ya mikono yako.

This is it, ilikuwa ni movie ambayo nimeipenda sana, ilikuwa ni ya kiaina yake hasa hao watoto kwa kweli walimudu sana characters zao. Nina imani hii film inayokuja na wao wakiwemo itakuwa ni nzuri zaidi, I cant wait to see it. Mungu azidi kukubariki.

Anonymous said...

Upo juu babake no mpinzani tunasubiri kwa sana tuione. Keep it up!!!
Mama Mario

Anonymous said...

Kanumba mimi naomba nikushukuru sana kwa kuwaelimisha hawa watoto wetu. Thank you na kazi zako ni nzuri sana, MUNGU akusaidie zaidi ya hapo yaani sio Kampuni wala vifaa atakupa uwezo zaidi kwani kila amtegemea yeye atamtia nguvu. Tupo pamoja. Sahbiki wako namba moja hapa.
Mama Mario

Anonymous said...

Niliiona This is it. Hakika Jenifer alikusumbua Anko.JJ. nasubiria na hii. Mdau-Lil Holland

Anonymous said...

daaahhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!HONGERA SN KAKA UMEJITAHIDI MNO...HII FILAMU ITAITWAJE???MANA NAISUBIRI KWA HAMU I THINK ITAKUA KALI ZAID YA THIS IZ IT.... CONGLAT......

rachel said...

Kanumba hao watoto hawaendani kabisa na hayo mazingira ya kijijini wanaonekana kabisa wanaigiza. we need to see something reality hata kama ni filamu. mmeshindwa kuwafanya waendane na hayo mazingira? japo kwa nguo! mbona wewe umeweza?

Anonymous said...

Kanumba we ndo unafaa,mshauri mwenzio Ray kachukua vibinti anatudanganya eti watoto wale,

Anonymous said...

big up!!!!!!! one love brother.

Anonymous said...

am diying waiting for the film. God bless you kijana. film za bongo hazinipi hamasa ila this is it ilinikamata mpaka nikacheka. am waiting for the new one!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

am diying waiting for the film. God bless you kijana. film za bongo hazinipi hamasa ila this is it ilinikamata mpaka nikacheka. am waiting for the new one!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

thank you brother kanumba,but show the reality to that kids, see the village atmosphear..hebu wavalishe mavazi ya kijjini waongeze uhusika zaidi...........TUPO PAMOJA,MORER THAN BLESSING,GOD BE WITH YOU IN YOUR WAY.ASANTE.