Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Sep 4, 2010

SAKATA LA SIMU KUUA LAMTATIZA THE GREAT

Toka jana kumekuwa na msg ambazo tunatumiwa katika simu ambazo kwangu zimekuwa nyingi sana zikisema..''Ukipigiwa simu kwa private number au ikiandikiwa call kwa red colour usipokee ni mionzi unaparalise na kufa.Imetokea Kenya na watu wamekufa.Julisha ndugu na jamaa wote''Sasa asubuhi ya leo nikawa napata simu nyingi zikiandika call ila kwa maandishi meusi kitu ambacho nimekizoea maana mara kwa mara hupokea simu za namna hii toka nje lakini kutokana na msg hizi zilizokuwa zikitumwa nikajikuta sipokei toka asubuhi mpaka majira ya jioni baada ya kusoma gazeti fulani lililosema kuwa ''TCRA YAKANUSHA UVUMI ULIOENEA KUWA SIMU KUUA''Ndipo nikaamua kupokea simu hizo ambazo toka asubuhi zilikuwa zikipigwa kwa wingi maskini hata nilipopokea simu niliiweka mbali na sikio na kuweka loud speaker cha kushangaza kumbe ilikuwa simu ya kazi toka India nikaumia sana maana walinilalamikia kuwa toka asubuhi walikuwa wananipigia sipokei.AMA KWELI SAKATA HILI LA SIMU KUUA LIMENITATIZA.

3 comments:

Anonymous said...

pole sana kakangu,hizo ni porojo tu.mimi ni mkenya na sijaona wala kushuhudia mtu amekufa kwa sababu hizo.jamani watu wanamabo duh!sikujua pia TZ zitafika.ningewajulisha toka wiki jana.

Anonymous said...

i don't think so,may be.

BQ said...

WE NAWE EMBU USITUTIE AIBU KWANI WE ULIAMAINIJE ULE UZUSHI?YAANI KABISAA ULIAMAINI ETI UKIPOKEA UTAKUFA UNGEJIULIZA KWANZA HOW JAMANI, POLE SANA