Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Sep 25, 2010

UZINDUZI WA FILAMU YA BLACK SUNDAY MLIMANI CITY NI WA KIPEKEE TANZANIA

Kwa mara ya kwanza katika historia ya filamu za kiswahili za kitanzania,filamu hii ndio inafungua dimba na kuwa filamu ya kwanza ya kibongo iliyochezwa na mimi The great pioneer kuoneshwa katika jumba la sinema ambapo tumezoea kuona filamu za nje tu zikioneshwa humo lakini hii imeweka historia nzuri.Ilizinduliwa juzi mlimani city na imeandaliwa na kampuni ya PILIPILI ENTERTAINMENT na Washiriki ni STEVE KANUMBA,MONALISA ,YUSUPH MLELA,MZEE CHILO,AUNTY EZECKIEL nk.Picha chini ni matukio ya uzinduzi huo jinsi ulivyofana.Huku mgeni rasmi akiwa ni mtoto wa raisi MIRAJ KIKWETE. Tuliingia kwa gari hilo linaloonekana hapo kabla ya kukanyaga red carpet

Mara baada ya kushuka katika gari tukakanyaga kitu chekundu hapo,The great na Mlela pamoja na ma boss wa kampuni ya Pilipili.

Tukisonga mbele The great na MR.Nilesh mkurugenzi mkuu wakampuni ya pilipili

Zamaradi toka Clouds tv akimuhoji mzee Mlela na mwanae Yusuph Mlela

Bazo toka TBC1 akimuhoji The great katika red carpet juu ya pamba alizopiga kuanzia kiatu mpaka nywele

Director wa movie hii ya BLACK SUNDAY MR.Sameer Srivasta akiulizwa maswali kadha wa kadha na Zamaradi

Director wa movie ya PAY BACK na NANI,MRS SAJNI SRIVASTA toka pilipili akihojiwa katika red carpet

Mgeni rasmi ndg.Miraj Jakaya Kikwete akipeta katika kitu chekundu huku bazo akihoji mawili matatu

Zamaradi akitwanga maswali kwa the great

Natasha na Mlela

Wa kwanza kulia Mr.Vinod ndie cameraman aliyeshoot movie hii ya BLACK SUNDAY

Mlela,Jimmy master,The G,pioneer

Cheni,natasha ,kanumba the great

Umati wa watu waliofika.

Swahiba na zamaradi

The great na Sauda toka star tv.Toka kulia ni Raisi wa shirikisho letu la filamu(TAFF) Simon Mwakifamba nae alikuepo

wadau

Sauda akimhoji mtoto huyu ambaye nae kashiriki katika filamu hii

4 comments:

Amina Zangira said...

saafiiiiiiiiiii sana uncle jj hiyo movie nimebahatika kuiona ila inatisha pale ulipopeleka taulo na pipi kifua duuuuuu nimewakubali pilipili kiasi fulani ila wakaze buti.

Juma said...

Kanumba samahani nikuulize swali na tena naomba unijibu,,huyu bwana Jimmy master kwasasa kuna filamu nyingine ambayo ameshazitoa baada ya zile za misukosuko?Kwasasa yeye anajishugulisha na nini?Asante,huyu bwana nilipenda anavyoigiza kwakweli.Samahani naomba jibu kanumba.

Anonymous said...

hongereni kwa kuzindua new albumhuyu sauda aache kujichuna sasa, na huyo zamaradi miguu kha! kazi kwelikweli.

Anonymous said...

huyo zamaradi amekuja hapo kama mwalikwa au amekuja kama mwandishi wa habari toka clouds tv mbona hatumuelewi? mwandishi wa habari na hicho kinguo jamani wapi na wapi au hiyo clouds tv haina viongozi na watu waliobobea ktk mambo ya tv walisha zoea tu radio?