Baada ya kumaliza vizuri maonesho yetu mjini Bukavu-Congo tulielekea mjini Goma mji mwingine ulioko nchini Congo,huko mapokezi yake yalikuwa zaidi ya Bukavu.Huku nako watu 5 walilazwa hospitali kwa kuumia,na mtu mmoja alifariki dunia.Pia inasemekana wanawake 7 waliachwa na waume zao kutokana na kwamba waliwaacha watoto nyumbani na nyumba zao kuja katika onesho kutuona. Mtoto Jennipher akihojiwa na wana habari,kushoto ni mama Vero mwenyeji wetu,kulia swahiba.
Furaha kwa mapokezi mazuri
Msafara barabarani ulikuwa hivi.Tathimini mwenyewe ni kiasi gani sanaa hii ya filamu tulivyoitangaza ndani na nje ya nchi,Huku tunasimama kama ma balozi wa nchi yetu tukipepea bendera yetu kupitia filamu zetu.Swali Je Serikali yetu inayatambua haya?Viongozi wetu wanayajua haya?kama wanajua mbona kimya kutetea kazi zetu za filamu?kama hawajui ni kwanini hawajui wakati wapo hapo kwa ajili yetu?
1 comment:
Jamani kwani hao wadada ni lazima wavae hivo ndo kuonesha kwamba wao ni wasanii wa juu au?? ukiangalia na sehemu mlizokuwa mkienda hayo mavazi ni tofauti kabisa, mnatakiwa mjue wapi pa kuvaa nini jamani,supastar sio lazima avae skimpy clothes ndo awe tofauti na watu wengine,endapo ni utofauti mnatafuta na si vinginevyo!!!!
Post a Comment