Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Dec 20, 2010

ZIARA YETU NCHINI CONGO katika uzinduzi wa filamu yetu ya OFF SIDE.

Jumatano iliyopita saa sita za mchana,The great,swahiba,Jenifa,Johari,Aunty na uongozi wa STEPS tulielekea nchini Congo kupitia KIGALI-RWANDA katika kuzindua movie ya OFF SIDE,Blog hii inakuletea matukio ya safari nzima na jinsi ilivyovunja rekodi kwa umati wa watu na mapokezi ya nguvu,mpaka sasa bado tuko huku Congo na hali imekuwa ni ya kushangaza. Tukiwa uwanja wa MWL JK Nyerere tukisubiri kuondoka

Ndani ya ndege Johari,Jennifa,na Aunty katika pipa kwenda Congo kupitia Kigali

Pritesh kushoto na Jairad kutoka Steps

Me na Swahiba pipani

Jennifa alianza kutapika wakati ndege ilipoanza kushuka

Tukiwasili uwanja wa ndege wa Kigali na mapokezi yakawa hivi

Katika basi tukitoka airport sasa Jennifa yuko fiti hatapiki tena

Mashabiki walifunga mitaa na barabara kwa kutupokea kwa shangwe

Umati umetuzunguka na kutufata popote tuendapo

Umati mkubwa wa watu,barabara na mitaa imefungwa huku ulinzi wa polisi ukiongezwa kila mara kutokana na watu kujaa sana barabarani na kusababisha foleni kubwa sana ya magari

Nikihojiwa na waandishi wa habari toka magazeti,radio na tv mbalimbali za Rwanda

Umati mkubwa sana wa watu(mashabiki)wakitushangilia...NITAENDELEA KUWAJULISHA YANAYOJILI HUKU HIVYO TEMBELEA BLOG HII KILA WAKATI MAANA NI BALAA

3 comments:

Albert said...

Mbona siamini Bro? Kumbe kazi zenu zinakubalika kiasi hichi? Siku mtakapofika huku ma juu hali itazidi hiyo ya Rwanda kwani hata huku kazi zenu tunazi appreciate sana.
Endelea kutupa news kuhusu safari hiyo tuko nanyi 24hrs!
Albert
Western Australia.

Anonymous said...

kanumba katika picha ulizochemsha THE MORNING ALARM ndio inaongoza yaani story haieleweki,production zero na ndefu sana mpaka inabore,kwakweli si filam yako ya kwanza kwa ubaya...jaribu kupumzika sio kila mara unatoka filam ndio mana unachemsha!huwa napenda sana filam zako ni fana wako kabisa ila kwa MORNING ALARM..BIG NO!

Hadj Drogba "mwana chelsea" said...

kigali kusafi mpaka raha...sijui sisi tanzania na dar es salaam yetu tumekosa nini kwa mungu mpaka tukapewa laana ya uchafu kupindukia