Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jan 5, 2010

Ujio wa Ivory Coast nchini Tanzania...


Jana kulikua na kipute cha mpira kati ya Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephant) kilichofanyika katika uwanja wa Taifa Mkuu. Timu ya Ivory Coast imeomba kuweka kambi katika nchi yetu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la mataifa ya Africa yakayofanyika Nchini Angola kuanzia tarehe 11 mwezi huu. hii ni mechi ya kwanza ya kirafiki ambapo mechi ya pili watacheza na Rwanda katika uwanja huu huu siku ya Al'hamis kabla ya kwenda mashindanoni.

Watu wengi walijua kwamba  taifa stars tungepigwa 4 or 5 O'clock kutokana na hawa wajamaa kuwa na wachezaji walioshiba na maprofeshno katika kandanda. Lakini mambo yalikuwa siyo kama watu walivyodhani, drogba alitumia uwezo binafsi hadi kupata gori la kuongoza lakini huo mpira waliokuwa wanaupiga hawa watoto wa KIKWETE jamani tuache masihala, MPIRA TUNAUJUA. Sio kama ilivyokuwa miaka ya nyumba. Hasahasa kipindi cha pili wajamaa walianza kwa kasi kumbe si tulikuwa tunawasoma, si tukawachenjia kidogo kocha wao awatoe wachezaji wote awaingize tena wakina Drogba. (alituchezeshea vikosi viwili, kimoja kipindi cha kwanza na cha pili kikosi kingine jumla wachezaji 22)

kwa matokeo yangu ya harakaharaka sisi tungekuwa na magori 2 wao moja. Ngassa alikosa Gori la wazi yeye na kipa, na lingine Tegete alipiga mkwaju uliogonga mwamba na kurudi uwanjani....mpira Tumecheza sio mchezo.

No comments: