Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jun 27, 2011

JB APATA TUZO YA MUIGIZAJI BORA ZIFF....

Kupitia movie yake ya Senior Bachelor ktk bongo movie JB awa muigizaji bora...hongera kaka yangu tuendelee kupigana.....,Tuzo ingine ni ya marehemu Hammie Rajab aliyopewa kumuenzi kwa mchango wake ktk filamu hapa nyumbani... Tuzo maalum ya Hammie Rajab nilipewa mimi kumpokelea


JB akipokea tuzo yake


Akishukuru kwa tuzo na kusema tuzo hiyo ni maalum kwa mke wake ambaye amekuwa akimsalia usiku na mchana katika kazi yake ya uigizaji.


Pilipili nao walichukua tuzo ya movie bora iitwayo RAY OF HOPE


JB na tuzo yake kwa furaha,,

4 comments:

Anonymous said...

hongera sana kaka hiyo tuzo umeipata kihalali kabisa hata mimi ninakukubali ile mbaya mungu akubariki upate tuzo zaidi ya hiyo.BIG UP sanaaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

Yaani kweli Mungu hamtupi mja wake, kweli kaka kazi unaifanya vizuri

Niwape ushauri tu kuwa tafuteni shule ili mjiendeleze ingawa vipaji mnavyo lakini shule muhimu ilimpate nagasi ya kuigiza na watu wa nje, tunahitaji kuona mabadiliko zaidi hasa katika kuchanganya vipaji, nashule ilimuweze kuigiza na watu wa nje.

Nendeni shule kaka zanguuuuu.

Hata wewe kanumba mimi nakukubali ila jiendeleze ili mpate radha tofauti tofauti wapendwa.

Kingine mukiigiza hebu jaribuni kuongea taratibu msipayuke maana inaonyesha kila kitu mnachukua kutoka Nigeria, wale ndivyo wanavyoongea sisi hatuongei kwa kupayuka ila tunaongea kwa utaratibu hata kama umepatwa na hasira unaonyesha hasira lakini si kwa kupayuka hatuko hivyo jamani.

Mfano movie ya Handsome wa kijiji ni nzuri ila swahiba wako amepayuka mno, pale alipotoka ngomani na yule mtoto akamkimbilia na kumsifia alivyoongea utafikiri alikuwa anagombana kumbe tu aongea kawaida kwa kumuuliza. vitu kama hivyo vidogo vidogo tu mrekebisho otherwise mnafanya vizuri sana.

RAFIKI YENU!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

huyu baba nampenda mno yani hakuna anemfikia hapo bongo kwa uigiozaji,unastahili kuipata

Anonymous said...

He deserve an award....