Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jun 30, 2011

SHEREHE YA KUMUAGA RAMSEY NOUAH ILIVYOKUWA.....

Mara baada ya kumaliza kushoot movie ya DEVIL KINGDOM kulifanyika hafla fupi ya kumuaga Ramsey na kumshukuru kwa ushirikiano wake wa hali na mali.... Me na Ramsey tukiingia sehemu ya tukio


Mkurugenzi wa Paradise city hotel akisalimiana na Ramsey


Patcho akiwa karibu na Ramsey,Patcho nae kashiriki vizuri katika movie hii na amekuwa na mchango mkubwa sana katika movie hii..


Hapo Ramsey anapewa salamu kwa Genevieve Nnaji,Ini Edo,Jimmy Ike,Omotola Jalade,Mike ezuruonye nk.


Mkurugenzi wa Paradise city hotel akitupa mawaidha yake mimi na Ramsey katika kufanya movie industry ya Africa kuwa juu,akishukuru kwa umoja na ushirikiano nilioufanya na Ramsey.

Picha ya pamoja na uongozi mzima wa hotel hiyo


Ramsey akishukuru na kusisitiza kuwa Africa ipo siku kabla hajafa kutakuwa na AFROWOOD,tutakuwa na industry yetu kama ilivyo nje,ipo siku mastaa wote wa Africa wa movie tutashiriki katika movie moja,leo hii Africa nchi zinazojulikana kwa movie sana ni Nigeria,Ghana na Tanzania hivyo tusiwadharau wasanii maana wanasimama kama alama na nembo za Taifa au kitambulisho.


The great nami nikatoa yangu,nikisisitiza movie industry tuiendeleze hadi watoto wetu waje wanufaike na kujivunia tuliyoyafanya hata kama tutakuwa kaburini lakini HISTORIA haitokufa.


Picha ya pamoja na wasanii wa movie na wadau wa movie bongo


Picha ya pamoja na uongozi mzima wa Paradise city hotel..

4 comments:

Anonymous said...

Besti hilo shati sasa basi, lipumzishe kidogo kama utachukia basi lakini imetosha

Anonymous said...

napenda unavyoigiza sana kanumba ila kitu kimoja nakuomba punguza kuvaa mashati ya maua na kuwakawaka duh! yani wewe na ray sijui ndo style mh haya wapendwa

Anonymous said...

lol kanumba watu wajanja hawashiki simu kiganjani ,wajanja simu wanaweka mkukoni mshamba atashika mkononi ajionyeshe anatumia ya aina gani

Anonymous said...

MI NAUSHAURI KIDOGO KWA NINI UNAPENDA KUVAA MASHATI YA KUNG'AA? PUNGUZA VAA MASHATI MENGINE UTAPENDEZA ZAIDI. HONGERA KWA KAZI NZURI NAKUPENDA SANA KAZA BUTI BRO