Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Jun 2, 2011

THE GREAT ATANGAZWA RASMI KUWA BALOZI WA OXFAM KATIKA KAMPENI YA OTESHA(GROW)

Katika ofisi za TGNP-Mabibo ndipo nilipotangazwa rasmi kuwa balozi wa Oxfam katika kampeni ya chakula ya OTESHA,lakini pia kampeni hii imezinduliwa rasmi duniani kote.Kwa ufupi tu OTESHA ni kampeni mpya ya OXFAM ya juu ya njia bora za kuotesha,kugawana na kuishi pamoja,ni kampeni yetu sote,mabilioni ya watu tunaokula chakula na zaidi ya wenzetu bilioni moja wanawake na wanaume wanaozalisha chakula hicho,ni kampeni yenye kutafuta suluhisho kwa mustakabali bora wenye uhakika wa chakula kwa kila binadamu. Mkurugenzi wa OXFAM bi Monica akinikabithi kitabu cha otesha mara baada ya kuzindua kampeni hiyo


Tukikionesha juu jinsi kilivyo chenye maelezo ya kutosha kuhusu Otesha


Nikipeana mkono na Mr.Silas mara tu baada ya kunitangaza rasmi kama Grow ambassador


Akina mama wakinishangilia na kunipokea kwa furaha baada ya kutangazwa


Furaha ikitawala mahali hapo


Nikikata utepe kuzindua rasmi kampeni hii


tayari upande mmoja


upande wa pili


Nikionesha jinsi gani akina mama wanavyoumia kulima kwa mkono huko vijijini tena katika ardhi wasiyomiliki


Kama balozi rasmi sasa nikishukuru kwa nafasi hii na kuhaidi kufanya kazi hii kwa moyo dhabiti kabisa.


Nikielezea ziara yangu niliyotembelea mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kahama na kijiji cha Mondo pia wilaya ya Kishapu kijiji cha Isoso jinsi watu wanavyoteseka na njaa hususani akina mama na watoto wanaokula mlo mmoja kwa siku tena hawashibi.


Kama balozi wa kampeni hii kauli yangu ni ...'''Mfumo wa usawa na endelevu wa chakula unawezekana,kwa pamoja tuondoe ukosefu wa usawa na haki za chakula katika familia zetu wakati tunapigana kubadili mfumo wa chakula duniani uwe wa haki kwa wote...''''by Steven Kanumba..katika kiingereza..'''A fair food system is possible,the one that is more equal and more sustainable,let's remove food injustice within our families as we change global food system to become fair to all...'''by Steven Kanumba.


Baada ya maelezo yangu kuhusu Shinyanga yaliyowagusa wengi nilishukuru na kuwapungia mkono..


Waliniomba niwasogelee kwa karibu ili wanione vizuri nami sikusita kufanya hivyo


Niliwasogelea kila upande kukata kiu yao maana wamezoea kuniona katika filamu tu


Nikisaini katika bango hilo na kuruhusu kila mtu asaini hapo ishara ya ufunguzi mwema


Picha ya pamoja wote kuanzia wafanyakazi wa TGNP,OXFAM na wadau mbalimbali


Tulimaliza kwa kupata mlo kamili kama unavyoona the great mbele akifuatia Bi Monica(Oxfam country Director)

9 comments:

Anonymous said...

Uko juu tu sana kaka.napenda maendeleo yako.kila siku unapiga hatua moja mbele.mwenyezi mungu akuzidishie.

Anonymous said...

bro uko juu vibaya mno jina la bwana libarikiwe.

Anonymous said...

Congratz kanumba sasa nakuomba ukae chini utoe movie inayoonyesha hali hali ya Mtz maana Viongozi wao hawalitambu hilo na baadhi ya watz kuwa kuna watu wanaishi kwa kupumulia Oxygen nina maana walalalia maji au mlo 1

Anonymous said...

hongera kanumba kwakuchanguliwa kuwa balozi wa oxfam roho yako nzuri sana ndio maana mungu anazidi kukufungulia milango endelea hivyo hivyo achana na wale wenye roho ya kwanini ambao kazi yao ni kuwakatisha wenzao tamaa usijali hizo unazokutana nayo ni challenge zitazidi kuku sukuma mbele zaidi na mafanikio zaidi napenda kazi zako nakupenda na wewe mwenyewe japo sikujui lakini roho yako inaonekana ni nzuri sana mungu akubariki nakutangulie kwa kila jambo ulifanyalo

Anonymous said...

kanumba ungekuwa unavaa nguo za kawaida jamani,the dress was ok the shoes BIG NO NO Mr.Bin,Bella naija siku waliona picha yako wakacomment is that Tanzanian artist used to wear funny clothes

Anonymous said...

sasa uoe kaka na heshima itazidi kuongezeka zaidi na zaidi

Anonymous said...

Kanumba mdogo wangu wewe ni kati ya waigizaji ninaoona fika watafika mbali. Unafanya vizuri sana ku network na wanigeria kwani wao wako more advance. Big up, I can see a bright future ahead of you.

joff Mulenga said...

yes we real appreciate what your doing bro ,you run this Tanzania

joff Mulenga said...

kaka thanks God umepiga hatua kubwa sn kwa hii tansia ya filam hapa Bongo ,kufanya move na Ramsey ni hatua kubwa zaidi ya kuendelea kizitangaza kazi zako level nyingine zaidi,BIG UP YOUR SELF