Katika ofisi za TGNP-Mabibo ndipo nilipotangazwa rasmi kuwa balozi wa Oxfam katika kampeni ya chakula ya OTESHA,lakini pia kampeni hii imezinduliwa rasmi duniani kote.Kwa ufupi tu OTESHA ni kampeni mpya ya OXFAM ya juu ya njia bora za kuotesha,kugawana na kuishi pamoja,ni kampeni yetu sote,mabilioni ya watu tunaokula chakula na zaidi ya wenzetu bilioni moja wanawake na wanaume wanaozalisha chakula hicho,ni kampeni yenye kutafuta suluhisho kwa mustakabali bora wenye uhakika wa chakula kwa kila binadamu. Mkurugenzi wa OXFAM bi Monica akinikabithi kitabu cha otesha mara baada ya kuzindua kampeni hiyo
Tukikionesha juu jinsi kilivyo chenye maelezo ya kutosha kuhusu Otesha
Nikipeana mkono na Mr.Silas mara tu baada ya kunitangaza rasmi kama Grow ambassador
Akina mama wakinishangilia na kunipokea kwa furaha baada ya kutangazwa
Furaha ikitawala mahali hapo
Nikikata utepe kuzindua rasmi kampeni hii
tayari upande mmoja
upande wa pili
Nikionesha jinsi gani akina mama wanavyoumia kulima kwa mkono huko vijijini tena katika ardhi wasiyomiliki
Kama balozi rasmi sasa nikishukuru kwa nafasi hii na kuhaidi kufanya kazi hii kwa moyo dhabiti kabisa.
Nikielezea ziara yangu niliyotembelea mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kahama na kijiji cha Mondo pia wilaya ya Kishapu kijiji cha Isoso jinsi watu wanavyoteseka na njaa hususani akina mama na watoto wanaokula mlo mmoja kwa siku tena hawashibi.
Kama balozi wa kampeni hii kauli yangu ni ...'''Mfumo wa usawa na endelevu wa chakula unawezekana,kwa pamoja tuondoe ukosefu wa usawa na haki za chakula katika familia zetu wakati tunapigana kubadili mfumo wa chakula duniani uwe wa haki kwa wote...''''by Steven Kanumba..katika kiingereza..'''A fair food system is possible,the one that is more equal and more sustainable,let's remove food injustice within our families as we change global food system to become fair to all...'''by Steven Kanumba.
9 comments:
Uko juu tu sana kaka.napenda maendeleo yako.kila siku unapiga hatua moja mbele.mwenyezi mungu akuzidishie.
bro uko juu vibaya mno jina la bwana libarikiwe.
Congratz kanumba sasa nakuomba ukae chini utoe movie inayoonyesha hali hali ya Mtz maana Viongozi wao hawalitambu hilo na baadhi ya watz kuwa kuna watu wanaishi kwa kupumulia Oxygen nina maana walalalia maji au mlo 1
hongera kanumba kwakuchanguliwa kuwa balozi wa oxfam roho yako nzuri sana ndio maana mungu anazidi kukufungulia milango endelea hivyo hivyo achana na wale wenye roho ya kwanini ambao kazi yao ni kuwakatisha wenzao tamaa usijali hizo unazokutana nayo ni challenge zitazidi kuku sukuma mbele zaidi na mafanikio zaidi napenda kazi zako nakupenda na wewe mwenyewe japo sikujui lakini roho yako inaonekana ni nzuri sana mungu akubariki nakutangulie kwa kila jambo ulifanyalo
kanumba ungekuwa unavaa nguo za kawaida jamani,the dress was ok the shoes BIG NO NO Mr.Bin,Bella naija siku waliona picha yako wakacomment is that Tanzanian artist used to wear funny clothes
sasa uoe kaka na heshima itazidi kuongezeka zaidi na zaidi
Kanumba mdogo wangu wewe ni kati ya waigizaji ninaoona fika watafika mbali. Unafanya vizuri sana ku network na wanigeria kwani wao wako more advance. Big up, I can see a bright future ahead of you.
yes we real appreciate what your doing bro ,you run this Tanzania
kaka thanks God umepiga hatua kubwa sn kwa hii tansia ya filam hapa Bongo ,kufanya move na Ramsey ni hatua kubwa zaidi ya kuendelea kizitangaza kazi zako level nyingine zaidi,BIG UP YOUR SELF
Post a Comment