Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Apr 20, 2010

Baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi leo kuhusu movie yetu nilielekea ofisini kwa ANKAL kumsalimia safari ilikuwa hivi.

Baada ya kufika MR.Iman Man akanidaka ili anipongeze kwa kazi zangu lakini pia alinihoji kwa ajili ya makala yake ambayo itatoka hivi karibuni.

Hapa nikiwa nimeshafika ofisini kwa ANKAL ambaye ndiye mwasisi wa mambo ya blog lakini pia huwa ni mshauri wangu mzuri sana leo nikaona nimtembelee kidogo.

Hapa nikiotea sijui yupo au lah?

Nikapandisha ngazi bwana

ANKAL ni mheshimiwa bwana hivyo lazima usaini kabla ya kumuona

Kutokana na haraka niliyokuwa nayo ya kuwahi mkutano na wandishi nilisahau kuvaa mkanda hivyo wakati natoka kwenda kwa ANKAL huyu kijana akaniona jinsi suruali iko wireless akaning'ang'aniza ninunue mkanda toka kwake nami nikaona si jambo baya kijana alifurai sana maskini maana nilimpa pesa mara mbili ya ile aliyotaka,niligundua pia ni shabiki wangu mkubwa sana.

Nikimtolea pesa kijana kwa ajili ya kununua mkanda wa suruali toka kwake

Hapa ndipo alipoanza kuniuzia mkanda lakini nadhani aliiona suruali yangu kuwa haikuwa sawa kiunoni,Nashukuru Mungu waandishi wa habari hawakuniona maana nilivyokuwa naizuia hata wewe usingejua.

2 comments:

BQ said...

HA HA HA UWIIIIIIII NDO MAANA INATAKIWA UOE MAMBO KAMA HAYA KUNAKUWA NA MTU WA KARIBU ANAYE KU GUIDE, POLE MA DIA

Anonymous said...

Nizungumzie hapo ulipokaa na Ankal. Ankal yuko makini sana na kazi yake huwezi kuchangia kitu saa tatu eti hadi jioni hajakitoa ni mwiko. Lakini Kanumba hhatusemi hutoi ila unachelewa sana kuto maoni yetu. inakuchukua hadi wiki maoni hujatoa hii si nzuri.Ankal unatoa maoni saa tatu asubh na saa tano ameshaingiza. Jaribu kumuiga utakuwa juu.kama yeye.