Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Apr 17, 2010

MAMBO BADO KAZI NDIO KAMA INAANZA NA PILIPILI ENTERTAINMENT CO LTD

Yusuph Mlela na Monalisa katikati ya scene ndani ya casino.

Cameraman akiwa kalala chini akiwarekodi mona na mlela

Wakati wa msosi eti mdogo wangu Yusuph mlela akataka kupimana ubavu na mimi katika makulaji wewe tizama sahani zetu uone

The great nikitubu dhambi katika sehemu maalum ambayo hutumiwa na wahumini wa Roman catholic katika kuungama dhambi hii ni katika movie hii,mojawapo ya scene.

Hapa nikifundishwa jinsi ya kucheza kihindi au ki Amita bachan

Nikijahidi kuzishika step

Hapa director Sameer akiset mwanga wa taa kwa kushirikiana na crew yake

Mara kwa mara tunapomaliza kushoot scene tunapewa mda wa kupreview kuona tulichokicheza

Hapa uongozi wa Pilipili Enterntaiment kwa pamoja na The great,Mona na mzee Chilo.

The great na MR.Niresh Bhat mkurugenzi wa kiwanda cha African pride na ni mmoja wa wakurugenzi wakuu wa Pilipili entern..alikuwa Nairobi mara baada ya kupewa taarifa kuwa nimekubali kufanya kazi na kampuni yao alisafiri upesi kuja location nilipo na kuongea zaidi na mimi na tukapiga picha ya pamoja,mara nyingi huwa sipendi kufanya kazi na kila kampuni ya filamu bali huwa nachagua na moja ya vigezo ambavyo huwa naviangalia mbali na malipo lakini huwa naangalia story,script,casting,director,crew ya production,vifaa na ubora wake,promo ya movie itakavyokuwa,schedule ya kazi yenyewe nk,nikiridhika kama hivi ndio utaniona location kama ninavyoonekana hapa sasa,MR.Niresh alisifia sana movie yangu ya Family tears akasema ni best family movie at all time,akasema miezi sita nyuma amekuwa akifatilia rekodi yangu ya kazi katika movie ndipo wakashawishika kushirikiana na mimi kwa hii kazi yao nami nawapa ushirikiano wa dhati kabisa.

Huyu ni cameraman wa pilipili MR.Vinod anayeshoot movie hii jamaa ni mkali sana katika camera katika kumuuliza CV yake ameshashoot movie kadhaa Bollywood mana ametokea hukohuko tena kwa kutumia filmcamera.

Unaweza kushangaa hii taa imewashwa huku nyuma katika dirisha na pikipiki iko hapo ukadhani havina kazi kumbe vina kazi kubwa sana kuna mwanga fulani umetengenezwa hapo unaotoka hapo na kukutana na mwanga wa ndani hivyo pakatengenezwa hali fulani kama alfajiri panapotaka kupambazuka...


2 comments:

ngaizaskids said...

kazi njema kakangu, na hao wengine. zidi kutuwakilisha.

kokusima

Anonymous said...

Ama kweli bongo hakuna diet. Mimi nilidhani kanumba mwili wako unauweka fit{kwani una mwili mzuri}kumbe unafakamia kula hivyo?maana hicho chakula kimejaa. Na hemedi nae katika interview moja alisema kwa siku anakula kuku 3,na anapenda kula mno. mmh