Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

Apr 30, 2010

THE GREAT NDANI YA SAVANA LOUNGE KUONA MACHOZI BAND

Siku ya jana alhamis saa tano usiku niliamua kumtembelea dada yangu wa ukweli LADY JAY DEE na swahiba wangu wa siku nyingi CAPTEN GADNER G.HABASH pale SAVANA LOUNGE ambapo bendi yake BORA KABISA ya MACHOZI BAND hutoa burudani ya nguvu kweli kwa mashabiki wake wa ukweli kila siku za Alhamis hakika niliburudika sawia na nilipapenda sana kuanzia usalama wa magari katika parking lakini pia ndani ni kiwango unapata burudani bila ya jasho maana ubaridi mda wote wakupuliza vinywaji vya nguvu na watu wa maana lakini lililo kubwa zaidi ni namna bendi ya machozi band inavyokonga nyoyo toka moyoni na rohoni kabisa,hakika si pa kupakosa jamani wadau wa filamu nanyi mje kwa wingi ni vizuri kubadilisha mazingira. Mecky Macha a.k. mama wa lovely gamble,The great na Kajala tulikuepo hapo kupata burudani


mmmmmh mimi sijui?kwa mbali mkono wa kulia ni aliyekaa ni The big producer wa movie toka UK Mr.Allan Kallinga.


Nilikutana na mashabiki wangu wa ukweli bila fitna kushoto ni Upendo wa chanel ten wote hapo walikuwa wananambia kati ya filamu zangu ambazo haziwaishi hamu kila wakati ni RED VALENTINE NA VILLAGE PASTOR ILE MACHO KWA MACHO.

The great pioneer,Jide na wadau mbalimbali wa filamu na mziki kwa pamoja tukiburudika

The great pioneer,mdau kushoto na swahiba wangu wa siku nyingi capten G.HABASH kwa pamoja

My lovely sister Lady jay dee na mimi kwa pamoja,pengine mnaweza kuuliza kwa nin i namuita my lovely sister,wote ukiangalia historia zetu tulikotoka au kuanzia ni Shinyanga,na kali zaidi ni kuwa shule ya msingi aliyoanzia JIDE ndipo namimi nilipomalizia hapo Shinyanga japo alikuwa kanitangulia ni Bugoyi primary school,ni mchapakazi kama nilivyo mimi ni dada anayependa kuanzisha kitu ambacho hakijawai fanywa na yoyote katika historia ya mziki wa kisasa hapa home,hupenda amani,umoja na ushirikiano kwa watu wote kama mimi,husaidia wasiojiweza kama yatima maana tumeshakutana mara kadhaa katika changizo za watoto yatima tofauti na wasanii wengine,hapendi kuona mtu mnyonge akikashifiwa au kutukanwa kama mimi,pamoja na matatizo kadha wa kadha tunayopata kama binadamu au wasanii lakini bado huweza kusimama imara na kusonga mbele katika kazi kama mimi,kwa haya tu baadhi she is my lovely sister,She is my best friend.

Savana utakutana na watu mbalimbali mashuhuri hapa napo nilikutana na rafiki yangu Mheshimiwa Amosi Makalla hapo nilimtania kidogo kuwa jimbo la mvomero nitagombea mimi akanimbia kijana acha kabisa nimetoka kwa Obama kuchukua tuzo yangu ikiwa huko wamejua mchango wangu na kunikubali unadhani jimboni itakuaje nimeshashinda tayari nangoja tarehe tu ,nikamtakia kila heri mheshimiwa ambae nimeshawai kuhudhuria mkutani wake wa chama kule Reading-UK,Moja ya kauli zake ninazozipenda ni 'Ukiwa na roho mbaya sana enzi za ujana wako basi ukizeeka lazima uwe mchawi"''

3 comments:

lema one said...

tru8e bro filamu iliwika mpaka hapa kwetu savvana some hw nilikuwa nikifanya jambo ni macho kwa macho mpaka leo cool karibu tena nilikuona na wadada fagilia kwa wingiiiii mpaka basi ndo life letu ilo karbu sana paradise city hotel kama unataka vya kiafrika zaidi kila alhamisi saa moja mpaka nne tukimaliza tunaenda machozi band juu savvana launge

lema one said...

tru8e bro filamu iliwika mpaka hapa kwetu savvana some hw nilikuwa nikifanya jambo ni macho kwa macho mpaka leo cool karibu tena nilikuona na wadada fagilia kwa wingiiiii mpaka basi ndo life letu ilo karbu sana paradise city hotel kama unataka vya kiafrika zaidi kila alhamisi saa moja mpaka nne tukimaliza tunaenda machozi band juu savvana launge

Anonymous said...

Kanumba Bro i realy like u very much kama mdau wa films zako.napenda pia kuigiza.