Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 6, 2010

IFM wajiaandaa na uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (IFMso)

Chuo cha usimamizi wa fedha IFM ijumaa hii ya tarehe 7 May, watakuwa na uchaguzi mdogo (Primary Election) wa kuchuja na kupata wagombea watatu ambao wataingia katika uchaguzi mkuu wa wagombea watakaotoa Raisi mmoja wa Serikali ya wanafunzi inayojulikana kama IFMso (Institute of Finance Management Student Organization)

Katika nyakati tofauti chuo hicho kimekuwa kikionekana kukumbwa na migomo ya hapa na pale kwa madai ya wanafunzi wengi kutokuwa na imani na viongozi wanaowaweka madarakani kushindwa kutekeleza adhma ya wanafunzi kwa uongozi wa chuo hicho, je! viongozi wataochaguliwa katika uchaguzi huu watafanikiwa kufikia malengo na matakwa ya wanafunzi hivyo kuzuia migomo ya hapa na pale kwa kumaliza mambo yawahusuyo wanafunzi kidiplomasia? hilo mimi The great halinihusu wacha niwaachie wanafunzi wenyewe watajua nini cha kufanya zaidi ya kuwaombea kuwa na uchaguzi mwema na wenye kuleta Viongozi watakaowapenda na watakaowafaa.

No comments: