Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 16, 2010

MDOGO WANGU YUSUPH MLELA ANIALIKA MNUSO LEO NYUMBANI KWAO KINONDONI.

Leo jioni maeneo ya kinondoni rafiki yangu,mdogo wangu ambaye na yeye ni movie star tz ALINIALIKA home kwao kumtembelea na kumuona mama yake pamoja na kula msosi alionipikia yeye mwenyewe.Tulipata mda wa kuongea mambo kadhaa ambapo aliniambia mimi ni mtu aliyekuwa anani admire tangu zamani katika industry ya movie na bado anafanya hivyo,kaniambia planning zake katika sanaa anataka kuvunja rekodi yangu katika sanaa na kuvuka pale niliposhafikia,nilifurai sana kusikia kauli hiyo nami nikazidi kumpa njia kuntu za kufata ili azidi kung'aa,mlela ni moja ya ma actor wanaofanya vizuri sana na mwenye nidhamu ya hali ya juu location. hapa nikiwa chumbani kwake tukiongea nilimsifia sana kwa usafi wa chumba chake na jinsi alivyoweza kuweka mazingira mazuri ya anapolala maana kama msanii kitu cha kwanza hata kabla ya gari lazima ulale pazuri.

Mlela ebu punguza maswali nile huu wali jamani...


kazi ikaanza hivi..niliamua nijipakulie mwenyewe na tule humohumo chumbani maana kuna dvd tulikuwa tunaangalia

maongezi tukayakatisha kazi ikawa moja tu kuuuuuuuuuuuuuullllllllllllllaaaaaaaaaa

katika video tulikuwa tukimtazama Felix wazekwa mwanamziki wa congo ninayemhusudu sana

Baada ya msosi nilipata wakti wa kuwasalimia wazazi wa Yusuph Mlela hapa tukiwa na bibi yake Bi Hawa...alisifia sana kazi zetu.

MLELA,BI HAWA,MAMA YAKE NA MLELA BI MWANTUMU MGAYA NA MIMI THE G.

MLELA NA MIMI TUKIWA NA MAMA MZAZI WA YUSUPH MLELA MARA BAADA YA MAONGEZI NA CHAKULA,,,,ASANTE SANA MDOGO WANGU KWA MWALIKO HUU NIMEFURAI SANA KUWAONA WAZAZI HAKIKA TUMEWEKA URAFIKI WA KWELI NAMI NAKUAHIDI KAMA MAMA ALIVYOSEMA NITAKUSHAURI YALIYOMEMA ILI UFIKIE MALENGO YAKO KATIKA SANAA YETU

8 comments:

Anonymous said...

Kanumba,katika siku ulizonifurahisha,basi ni leo.Hiyo ni suprise ya nguvu kwangu mimi.kwani huyo Bi hawa ni ma maangu,nipo nje ya nchi kwa kweli nimefurahi kumuona.nimemwambia sister wangu yeye hajamuona mama etu kwa muda wa miaka kama 3 kumuona akaniambia machozi yalimtoka.Ahsante sana kanumba.

Anonymous said...

kwakweli nimefurahi, sana kumuona my mum please say hello to yusof and thank you kanumba i try to call you just to say thank you

Anonymous said...

kaka nakukubali sana ila unaniudhi kitu kimoja kitu chenyewe ni kutojali wasanii wa nje ya jiji kumbuka wewe ni star waukweli kwenye movie,mimi nipo korogwe- tanga wautu wakitokea kukuponda mtetezi nasimama kwani naipenda kazi yako nahitaji niwe kama wewe kwani sanaa ipo kwenye damu tatizo kwetu tabu hadi tamaa nakata.Napenda tuwasiliane,naitwa Mhina au Magwila kisanii

lily said...

yusufu wewe ni mkali nakufagilia sana kaka unanidhamu sana tofauti na yule anaekufatilia wewe mambo yako wewe ni big chipukizi .kaka wakisema usisikilize nakufagilia ile kishenzi wewe ni smart kama JUAN MIGUEL {WILLIAM LEVLY} yaani we acha tu ITS ME LILY KYARA .from kinondoni
.

Anonymous said...

SASA MASTAA WAKAKULA KITANDANI NA CHAKULA KINAWEKWA SAKAFUNI!?? KAMA MASTAA WANAISHI MAISHA HAYA JE WATU WAKAWAIDA ITAKUWAJE? MIMI SI STAA LKINI KANYUMBA NINACHO, KOCHI NINAZO NA NAKULA KWENYE DINING TABLE NA KAGARI KANGU KADOGO NINAKO!!! LAKINI NIKIPITA MTAANI HAO KINA KANUMBA NA MLELA NDIO WANAONEKANA WA MAANA NA MAGARI YAO MAKUBWA!!!AKILI NI NYELE KINA MTU ANA ZAKE, HAHAHAAAAAAAAAAAA!!!

LISA said...

MLELA ANAKAA USWAHILINIII KINONDONI MANYANYA HIYO NYUMBA YAO NI KAMA KAGOROFA FLANI UCHWARA HATA GARI HAIINGII KWA VICHOCHORO SASA SIJUI HUA ANALAZA WAPI GARI, SIMPONDI MAANA MLELA KIBINGWA HARINGI HAJIFAGILII NI MSAFI NATURAL NA NI MZURI USHAURI MLELA BADILISHA HOME KWENU AMA PANGA NYUMBA MDOGO WANGU SAWA

steven said...

Kaka kanumba napenda kazi yako mungu akuongeze myaka yakuishi duniani ok jina rangu steven blaiton naishi hapa marecan nataka tuwasiriane kupitia email. kanumbasteven@yahoo.com ok bayi sarimia yusuph.

steven said...

Kaka kanumba napenda kazi yako mungu akuongeze myaka yakuishi duniani ok jina rangu steven blaiton naishi hapa marecan nataka tuwasiriane kupitia email. kanumbasteven@yahoo.com ok bayi sarimia yusuph.