Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 13, 2010

...WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU MAANA UFALME WA MUNGU NI WAO(BIBLIA),TUWASAIDIE WATOTO WETU NA WADOGO ZETU(KANUMBA)

Kila mtu ana historia yake ama mbaya au nzuri ya enzi za utoto wake wapo ambao wakikumbuka nyuma wanalia na kuichukia dunia maana walikosa tumaini na faraja toka utotoni mwao.Leo hii sisi tuliokwisha ona angalau mwanga katika hii dunia ni vyema tukawa tumaini au faraja nzuri kwa watoto wetu,tukiwasaidia kuanzia malezi bora,elimu bora lakini pia kunyanyua na kuvumbua vipaji vyao ili kuvikuza waje kuwa zao jema ukubwani,wasije wakalia na kuichukia dunia kama wengine,ni jukumu letu kama wasanii ambao tumeshakuwa angalau wakongwe katika tasnia zetu kuwasaidia watoto wetu,wadogo zetu waendeleze yale mazuri yetu katika sanaa kwa manufaa ya jamii yetu yote.Jukumu hili si langu au lako tu bali ni sisi sote.Mimi kama Steven Kanumba nimeamua kuwashirikisha watoto katika filamu zangu kadhaa ikiwemo WHITE MARIA na THIS IS IT tena kama main character ili kuinua vipaji vyao ambavyo pengine bila sisi kufanya hivyo vitakufa bila kujua...Tusiishie tu kuponda kazi zetu na kuzidharau wakati mwingine tutizame na mazuri wayafanyayo wasanii wetu,itakuwa vizuri kama mchango wetu mkubwa tukauelekeza kwa watoto wetu maana huko ndiko zitokapo baraka toka kwa MUNGU.Ebu tuwasaidie,jiulize msanii ni mara ngapi umepita mtaani watoto wakakushangilia na kusema kuwa wanatamani kuwa kama wewe?kwangu inanitokea kila siku na kusema ukweli watoto kwangu ndio mashabiki namba moja,wakuonapo hawafichi hisia zao nami nawapa sapoti hivi kusaidia baadhi kwa kadri ya uwezo wangu.. Hapa ni katika This is it nikiwa na othman njaidi(kushoto)na kulia ni Khanifa Daudi.vipaji vyao hakika nimejaribu kuvionesha humu.


Hapa ni katika WHITE MARIA ebu tizama hili cover kwa juu ni watoto wengi ambao nimejaribu kuwapa nafasi nao kuonesha uwezo wao ili wanapokuwa wanajitengenezea mazingira hata ya ajira.

hapa ni katika WHITE MARIA

KHANIFA DAUDI ndiye kinara wa THIS IS IT sisemi mengi mtajionea wenyewe,hajawai kuigiza popote ila kwa hapa kavunja rekodi ya watoto wote.

OTHMAN NJAIDI yumo katika THIS IS IT naye kama kinara lakini pia utamuona pia katika WHITE MARIA

watoto hawa walikuwa wananipa hisia zaidi katika kuigiza jinsi nilivyokuwa nikiwafundisha na kuwaongoza walifanya hivyo hivyo bila ya kukosea

katika movie hii mimi ni mjomba wao tazama mapozi yao hakika tukiwapa nafasi wanaweza sana tusiwasahau jamani hata katika mziki huko

8 comments:

Anonymous said...

David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Imeisha hivi, Kanumba kamfumania demu wake aliyempata huko UK na jamaa kwenye kitanda chake, then anasikitika wale wako kwenye shuka wanamuangalia anavyolalamika, ehehehhe, dah! Sasa kumbe demu alikuwa na mume wake hakusema, kaja mpaka pale walipo na bunduki, nadhani kawaua wote
Yesterday at 2:50pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Imeisha hivi, Kanumba kamfumania demu wake aliyempata huko UK na jamaa kwenye kitanda chake, then anasikitika wale wako kwenye shuka wanamuangalia anavyolalamika, ehehehhe, dah! Sasa kumbe demu alikuwa na mume wake hakusema, kaja mpaka pale walipo na bunduki, nadhani kawaua wote
Yesterday at 2:50pm
Amani Lyimo
Amani Lyimo
muvi za kibongo michosho wanaigiza mpaka slow motion.@home watching F1
Yesterday at 2:50pm
Grace John Nyantori
Grace John Nyantori
Unadhani au ameua???
Yesterday at 2:51pm
Josef R. Sylvanus
Josef R. Sylvanus
wanacopy hadi maneno ya kuongea!
Yesterday at 2:52pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
G amenyanyua kupiga risasi picha likaisha, sasa labda kapiga ukutani, tusubiri part 2, unamfumania demu unaanza kushangaa, tena kwenye kitanda chako, mamae
Yesterday at 2:53pm
Grace John Nyantori
Grace John Nyantori
hahahaha si unaona wanaleta sababu tu ya part 2 mambo ya kizamaniii
Yesterday at 2:54pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
Na wanauza!!!!!!!
Yesterday at 2:54pm
Amani Lyimo
Amani Lyimo
Wanaiga kuigiza maigizo.ntajitahidi kupenda vyakwetu lkn sio hizi muvi.....
Yesterday at 2:59pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Tulilipishwa 6000, bilicana last week kwa ajili ya uzinduzi wa hii movie,tumeenda starehe zetu wakaanza kutuletea upuuzi wao, ebwana viatu ni chui chui Lily
Yesterday at 3:00pm
Mkunde Lily Edward
Mkunde Lily Edward
Hahaha yaan muv zote nlzowatch hzo ndo shuz zake,mbele mchongoko na kichui chui kwa mbal!na bado anapewa awardz et muigzaj bora!hate them muviz!muongozooo
Yesterday at 3:18pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
Kutana nao sasa ujionee vioja wanavyojiona ni superstars, actor n actress wa Tollywood
Yesterday at 3:22pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Tollywood my shoe, in english
Yesterday at 3:24pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
D ndo ivo .....Hollywood (USA), Bollywood (India), Nollywood (Nigeria) n now introducing Tollywood (Tanzania).
Yesterday at 3:30pm
Irene Mchomvu
Irene Mchomvu
Ha ha ha ha ha u made my day Davie!!!kuna hyo,DANGER ZONE,HOT FRIDAY,MY DREAMS.ndo ungetapika hata km hujala wali choroko!!!!
Yesterday at 3:49pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
I bet, hawaoni hata haya..

Anonymous said...

Hizi ni critics za movie zako katika facebook.. katika haya unaweza kupata mazuri yatakayo jenga tasnia yanko ya filamu kila la heri.....


David Samuel Marosi : all over the way to uk to act a crap movie, y wanaendelea kumdhalilisha Kanumba na english, movie kama audition, still watching it thou, LOVELY GAMBLE
Yesterday at 2:00pm via Facebook for BlackBerry · Comment · LikeUnlike
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
Unamzimia Kanumba ww
Yesterday at 2:04pm
Jackson I. Mwanyika
Jackson I. Mwanyika
Sema all the way to the UK kufanya maigizo...Ukisema movie nakuwa xcited halafu nikiona jina Kanumba naanza kukasirika..........Inakuaje kijana!!
Yesterday at 2:05pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
dah! An insult, but I will take it, na kwakuwa imetoka kwako, hujambo lakini?
Yesterday at 2:06pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
Mzima, sijui nyie?
Yesterday at 2:07pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Eheheheheh kaka hii aibu, wamekodi escalade ndefu kama coaster, halafu wamepanda wa3, halafu Kanumba kashuka kwa kuruka kama mtoto, anaingia kwenye meeting kama anaingia shule
Yesterday at 2:18pm
Mkunde Lily Edward
Mkunde Lily Edward
Am startn 2 imagn that muv!naomba niambie kavaa viatu gan?chui chui ama?hahaha!no bongo muv 4 me!wanahtaj muongozo loh!
Yesterday at 2:22pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Tena mkubwa, movie nzima wanazunguka UK, kwenye boti mara yale mabasi ya ghorofa, yaani full kero
Yesterday at 2:24pm
Grace John Nyantori
Grace John Nyantori
Movie zetu balaa tupu afadhali waongee kikwetu tu..
Yesterday at 2:29pm
Jackson I. Mwanyika
Jackson I. Mwanyika
Thats where me n' Ice come in...We gon make that kero go away!!
Yesterday at 2:35pm
Suzanne Nyakiamo
Suzanne Nyakiamo
He! Kwani r they acting in English?! Storyline ya igizo hilo ni nini? Kuiga is fine lakini kuiga bila mwelekeo is nt
Yesterday at 2:37pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
@ the end of the movie, D niambie kama jina la movie na yaliyomo yamo?
Yesterday at 2:38pm
Grace John Nyantori
Grace John Nyantori
Suzanne hujui hata ikiwa ya kiswahili the title is always in English mie ndio huwa wananiacha hoi
Yesterday at 2:38pm
David Samuel Marosi
David Samuel Marosi
Ebwana nimeipa tv kisogo, kuna mashindano ya kurap humo humo, wamewaweka jamaa zao wanaoishi huko, mara wanacheza video game, subtitle inachange to kiswahili to english, mchanganyiko wa lugha si mdogo
Yesterday at 2:44pm
Suzanne Nyakiamo
Suzanne Nyakiamo
He he he kwa kweli, davie tafadhali ebu tell us whether title na storyline zinaendana.ninavojua gamble ni kamari so i xpect scene kama casino.
Yesterday at 2:46pm
Lulu John Mduma
Lulu John Mduma
Suzzane waweza kuta they mean kuchezea penzi ka kamari....... Title za movie za kibongo mie ndo wanaponiacha hoi. Kuna moja "yellow banana".... Sikuona connection mpaka kesho!!! Loli!!
Yesterday at 2:49pm

mosisonia said...

Kaza buti kaka uko juu mtu wangu si unajua majungu lazima kwa mastar wakubwa kama nyie BIG UP KEEP IT UP MAN.

Anonymous said...

me mansubiri wema tu,(beautifully lady)
wa pili kanumba
wengine wafuate tu kama mkia,

walishaanza wameanza.
bye

anu narayan said...

hai,

wish you all the success for your effort...God bless you

:)

RENATUS KILUVIA said...

Nimesoma sana hizo comments zote hasa hizo ambazo zimetoka facebook na nimejifunza mengi,hao wote wanajifanya wasomi na ulaya wanaijua sana lakini kiukweli mi nawaona wote washamba tu,hata hizo movie za mbele ambzo wamekua wakiziangalia na kuona za maana ahawazijui pia,naomba wajiulize swali hili,movie industry hapa Bongo ina miaka mingapi mpk sasa??na hizo movie za Hollywood wanazozifagilia na industry nzima ya movie Hollywood ina miaka mingapi??wakishapata majibu hayo ndo waanze kuponda na kudharau kile ambacho watanzania wenzao wanajitahidi kukifanya,hata mbuyu ulianza kama mchicha,unaweza ukaenda shule na ku-graduate lakini usielimike,hawa jamaa wote waliokuwa wakichat facebook na kuponda movie zetu kama wame-graduate basi hawaelimika,wao wanataka nini??wanataka watanzania wafanye nini katika movie industry leo??wkt industry haina hata miaka kumi??industry mpaka sasa IMEPIGA HATUA KUBWA SANA,HUO NDIO UKWELI hata kama kuna baadhi ya watu hawataki,wengi wenye mawazo kama ya hawa ni WATUMWA WA KIFIKRA na MALAYA WA KIIMANI,wanaamini kizuri chochote hutoka ULAYA au kwa wazungu tu,POLENI NYOTE,na MUNGU AWASAMEHE SANA,mfano mzuri ni muziki wa BONGO FLEVA leo,ndio bado haujafika katika level za kimataifa,lakini walewale waliokuwa wakiuona muziki huu miaka kumi na tano iliyopita kama uchafu leo ndio wanaowalipa wasanii wa Bongo Fleva na wa Afrika Mashariki kwa ujumla dola kibao na kuwasafirisha kwenda ughaibuni kuwatumbuiza,ndo haohao leo wanajifanya wadau wakubwa wa muziki huo,huko ndiko tunakokwenda pia katika movie industry ya kibongo,juhudi zipo,watu wapo(wengine shuleni wakisomea),ideas zipo hivyo TUOMBENE UZIMA ili kila mmoja wetu ayashuhudie MFANIKIO ya industry hii kwa macho yake mwenyewe,HONGERENI na APPRICIATIONS nyingi kwa wanaharakati wote wanaolala MACHO wakifanya haya na yale kuhakikisha tunafika kule waliko HOLLYWOOD,TUSIKATISHANE TAMAA,TUPENE MOYO,mazuri ya MTANZANIA yeyote ni mazuri ya WATANZANIA WOTE,KANUMBA,RAY na wengineo please msikate tamaa,MWENDO MDUNDO,TUTAFIKA WADAU.

tuma said...

ana picha ya this it is yule mtoto wa kike iz very bright i like her she z sharp!

Anonymous said...

Bwana Renatus Kiluvia rudi shule ujifunze spelling kwanza