Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 26, 2010

BABU YANGU AFARIKI DUNIA USIKU HUU...

Ni yule ambae mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa 3 nilikwenda kumsalimia sasa amefariki dunia'Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la MUNGU wetu libarikiwe...amen,nakumbuka siku aliponiona alilia sana na kusema 'nilidhani nitakufa bila ya kukuona tena mjukuu wangu Kanumba''sasa nimekuona hata nikifa sawa'' hatimae yametia.. hapa siku aliponiona baada ya miaka mingi sana akalia sana nilipombembeleza anyamaze tukapiga picha hii.

hapa akilia sana kama mtoto mara gafla aliponiona akisema''nilidhani nitakufa kabla ya kukuona mjukuu wangu''marehemu babu yangu enzi za uhai wake aliwai kuwa daktari mkuu katika mikoa kadhaa kama mwanza,tabora nk,pia baada ya kustaafu alipewa cheti toka kwa aliyekuwa raisi wa awamu ya pili TZ Mh Ally Hassan Mwinyi cha kutoa huduma ya afya popote pale atakapokuwepo nchini katika kustaafu kwake kazi ambayo aliifanya mpaka mauti ilipokaribia kumchukua.


The great siku nilipotua kijijini kwenda kumsalimia babu....sifa na utukufu namrudishia mweza wa yote......GEHOVA

29 comments:

Baraka Mfunguo said...

POLENI KWA MSIBA MZITO. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.

Anonymous said...

Mh! Pole Kanumba,muhimu ulienda msalimia.Hapa kilichobaki ni tumuombee apumzike salama,na sisi tuombe kwa Mungu atupe maisha marefu tufike umri wake au hata zaidi.Kazi ya Mungu haina makosa.
Lil -Holland

de'victorious said...

pole sana kwa msiba wa babu mungu akup enguvu katika kipindi hichi kigumu........tuko pamoja...

Anonymous said...

pole sana,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema

frida said...

pole kwa msiba wa babu yako?
"ROHO YA MAREHEMU HILALE MAHALIPEMA PEPONI," AMINA.
Je alukuwa anaishi wapi babu?
si vibaya ukatuwekea picha za kwny msiba mara utakapo fika huko.
Rida.

Anonymous said...

Pole sana Kanaumba, may ur granddad's soul R.I.P

Anonymous said...

Pole sana Steve.Mungu alishikilia uhai wa babu mpaka muonane. Hope utakutana naye tena kwa Mungu siku ukimaliza safari yako vema. RIP babu, Mungu apokee kazi zako njema. AMEN, Mdau.

Rose said...

Maskini Babu naimani kila mtu anamkumbuka Pole kanunumba kwa msiba na mungu ailaze roho ya marehemu Babu mahali pema peponi Amen.

Anonymous said...

pole kanumba,
Mungu amuweke palipo pema babu yetu,
nasikitika kwakuwa tunawapoteza watu ambao ni muhimu sana kwenye maisha yetu, roho inaumba lakini ndio hivyo tena, wanasema kazi ya Mungu haina makosa.

Anonymous said...

Pole sana bro! Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi. Amina.

Albert said...

Pole sana bro!

Anonymous said...

pole sana kaka kwa kufiwa na babu. Yapasa umshukuru Mungu sana kwa kukupa wazo la kwenda kumuona kabla ya mauti yake. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina Lake libarikiwe

Anonymous said...

mh.....!!!
aisee pole sana kanumba jamani,
mpaka huruma sana, baba wa watu alivokuwa analia, pole sana kaka yetu. mungu ametoa na kutwaa,
jina lake lisifiwe.

aisha
tbt

Anonymous said...

Dar pole sana mr K, mungu amempenda zaidi ashukuruwe kwa kazi yako kubwa. Pole sana wote tuko njia moja ila kutangulia ndo ngumu, mdau kutoka Oslo Norway.

Anonymous said...

Kanumba mshukulu mungu sana kwasababu amefariki akiwa amekuona live nawewe umemuona tena live,,basi yoote ni kumuachia mungu kwasababu sote ndio njia,,kesho au kesho kutwa niwewe au mzazi au ndugu yako au mimi,kikubwa tu nikumsogerea mungu kila mwanya.Mungu ampokee mzee wetu huko ahela.Amen!

Anonymous said...

pole sana kwa kufiwa na babu,nakumbuka ulipo enda kumsalimu.yote ni mapenzi ya mungu.MWENYEZI MUNGU AMSAMEHE MAKOSA YAKE, AMWANGAZIYE MWANGA WA MILELE.AMENI

Anonymous said...

pole sana Kanumba, ni mipango ya mungu. Kama ulivosema jina la bwana lihimidiwe, yeye ndie muweza ya yote.

Poleni sana

Anonymous said...

Natumai hujambo,vipi mbona hatukuelewi maelezo yako? kijijini kwenu wapi? babu yako mzaa nani? kuwa wazi kwenye blog usituachie maswali.

Anonymous said...

pole sana kanumba Mungu aipi[umzishe roho ya marehemu mahali pema

BC said...

Pole kaka kwa msiba.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

MDAU NORWAY said...

pole sana kaka kanumba mshukuru MUNGU kwa kila jambo na baraka zote ulipata toka kwa babu ulipoenda mtembelea kabla hajafa .MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

Anonymous said...

Bwana alitoa na sasa ametwaa.
jina lake lihimidiwe.
Pole sana, hapa ndipo tunatakiwa kufanya mambo kama tunakufa leo, na kufanya mambo kama tutaishi milele.

Albert said...

Pole sana Kanumba kwa yaliotokea kwa familia yako. Kweli washabiki wako hapa Perth tulipokea habari hii kwa huzuni kubwa sana. Basi huu mzee wetu ambae tulimpenda kwa dhati, Mungu amlaze mahali pema! Haya yote ni maisha, na sisi wote ndo njia tutakayoipitia.
Albert
Perth, Western Australia.

Anonymous said...

Pole Kanumba...take heart dear and pray for him..."Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.........."

Do said...

Hallo Kanumba Pole na kufiwa na babu. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema. Astarehe kwa amani.

Anonymous said...

pole

Anonymous said...

Duh pole mwaya,,lakini naomba ubadilike tena sana,,,ni aibu kuona mademu unawaonga mipesa kutembea na wewe,,,lakini angalia mazingira ambayo babu yako alikuwa anakaa,,chumba kimoja mlango si kwambiii..cheki kochi,,kwa kweli babu yako hajaenjoy matunda ya mjukuu..embu badilika kabla hatujakubalikia...mwana mpotevu wee,,,

penina said...

Pole kanuba ungu akutie nguvu

penina said...

pole sana kanuba