Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 16, 2010

HAPPY BIRTHDAY MY BEST FRIEND,MY BROTHER VICENT KIGOSI(RAY)

Tarehe ya leo 16.5.2010 rafiki yangu na ndugu yangu wa mda mrefu swahiba RAY anatimiza umri wa miaka 30.mimi rafiki yako The great nakupongeza sana kwa hatua hiyo Mungu akulinde na azidi kukuongoza hasa katika malengo yako na ambayo kwa kiasi fulani unayatimiza sasa kasoro tu hilo la kuoa na kuwa na watoto ambao wengine watarithi na kuendeleza sanaa yako.Hongera sana rafiki yangu ni mengi umepitia na kupigana nayo na ni mbali sana mimi na wewe tumetoka japo wengi hawajui toka enzi twatembea kwa miguu,daladala,tax na sasa magari yetu wenyewe hakika ni mapinduzi ya dhati tumeyaweka si katika maisha tu bali hata katika tasnia yetu ya film ebu kumbuka mapinduzi yaliyotokea pindi tulipotoa filamu ya JOHARI,SIKITIKO LANGU,DANGEROUS DESIRE, hadi OPRAH,si hapo tu kumbuka mapinduzi tuliyowai kuyaweka katika tamthilia za ITV na TBC1 kama TUFANI,BARAGUMU,SAYARI,TASWIRA,RADI N.K...kumbuka film yetu ya kwanza kutengeneza iliyoitwa NENO(wengi hawajui)toka enzi hizo hadi sasa tumekuwa sugu katika gemu hili,MATUSI,DHARAU,KEJELI tulizowai kupata lakini Mungu kakupigania hadi sasa nakupa hongera sana hakika penye nia pana njia..am proud of u VINCET na zaidi mama yetu mama MARRY KIGOSI kwa ushauri na mawaidha yake ya kila siku(shukrani sana mama)tuzidi kuwa wamoja daima mimi na blog yangu pamoja na mama yako(mama kanumba..bi FLORA umeongea nae leo asubuhi umesikia mawaidha yake)Twakutakia maisha mema kumbuka hakuna safari iliyokosa kona.........JAMANI TAFRIJA YAKE TUTAIFANYA JUMATANO WIKI HII WAALIKWA WOTE MSIKOSE KUHUDHURIA.....the GREAT nitakuepo kuhakikisha inakwenda vizuri maana swahiba ameshanifanyia party kadhaa za birthday zangu na kusimamia...karibuni sana. SWAHIBA KATIKA POZI LA KI BIRTHDAY

TULIKOTOKA NA SWAHIBA KIKAZI HAPA ILIKUWA ZANZIBAR KATIKA SHOOTING YA MOVIE YA OPRAH


MATUKIO KADHAA YA KISANII LAZIMA UTATUPNA TUKO PAMOJA NA SWAHIBA NI NADRA SANA KUTOTUONA PAMOJA TIZAMA HAPA..

MFANO WA BAADHI YA MATUKIO AMBAO HUONGOZANA PAMOJA NA SWAHIBA..ONCE AGAIN HAPPY BIRTHDAY RAY

7 comments:

Anonymous said...

nimefurahi sana kanumba ulivyo karibu,ushirikiano na mapenzi ya dhati kwa mwenzio ray mwendelee hivyohivyo msiingiwe na ibilisi mtaharibu kila kitu,nimetoka kumwandikia sasa hivi ray,big up wote wawili.ni mimi mdau kutoka marekani

Anonymous said...

Kanumba mdogo wangu jifunze kuandika majina ya watu kwa ufasaha, ...Mfanano, "MARRY" ni verb na maana yake waijua bila shaka! Usitegemee MARRY kuwa jina la mtu. Jina lenye matamshi kama hayo but spelling tofauti ni Mary au Maria! Anyway, hongereni sana kwa mafanikio yenu na Happy birthday kwa ViKi! Mdau.

Anonymous said...

pamoja na watu kuwapondeni! kuwakatisha tamaa! kuwakajeli! Bado hamkufa moyo! Hongereni sana kwa hilo, Mungu azidi kuwapa nguvu na moyo wa upendo msimpe nafasi Ibilisi hata kdgo! Napenda sana movie zenu ingawa huwa nazipata kwa nadra sana! napenda mnavyojituma!NAWAPONGEZA SANA! pia msisahau kumshukuru Mungu kila kuitwapo leo. Dada yenu Washington DC

Anonymous said...

misifa tu watu wangine bwana. Unatoa risila nyiingi utazani Ray kafa kumbe ni BD tu.

Anonymous said...

Wewe nawe unapenda kusifiwa tu unabania comment, kama hutaki maoni ulifungua ya nini

lea said...

jamani hizo pic za b'day ya ray mbona huzipost?
Lela.

Anonymous said...

Aisee cna la kuongea zaidi kuwapongeza kwa kazi zenu nzuri pia nakupongeza kaka kanumba kwa kuendekea kumjali swahiba wako endeleeni kupandana jaman mcckilize maneno ya watu kuna binadamu wengine hawapendi kuona watu wanapendana co cri kk kanumba nazifeel kazi zako kiukwel tokea ulivoingia tu kwenye tasnia hii ya sanaa cwez kuangalia film yyte ya kibongo kama ww au ray kwenye film hiyo hayumo kwenye film hiyo vilevile ushauri tu mjipange na kutupa mambo mapya ktk film zenu kama film ya this is it yan iko unique na hivyo ndivo film inavotakiwa kuwa. mwisho wish U KAZ NJEMA TS UR YOUNG SIS FRM UDSM