Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 19, 2010

THE GREAT AKUTANA NA NABII TITO...waronga kwa masaa kadhaa.

Leo nimekutana na nabii Tito ambaye amekuwa maarufu sana kutokana na mawaidha yake anayopita barabarani akihubiri,Nabii Tito akasema alikuwa ananitafuta sana mara baada ya kukutana na swahiba wangu RAY hivyo akasema ilikuwa bado mimi,lakini kwangu lengo lake lilikuwa eti kwa sasa yeye anatafutwa sana kuuawa na kuna watu wanamtishia maisha yake hivyo akanambia kwakuwa mda wowote yeye anaweza kutoweka duniani iwe kwa kuuawa au kimaajabu anaomba eti iwapo atatoweka basi eti mimi The great niendeleza mafundisho yake kwa jamii nzima kulingana na imani yake. Nabii Tito alinambia kuwa yuko karibu kufungua kanisa lake ambalo waumini wote lazima wawe wanakunywa pombe maana ni tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na hata biblia kwa mujibu wake haijakataza sema watu wanazidisha kuliko kile kiasi kilichozungumzwa ...hapa alinifunulia biblia timotheo 5:25.

Hapa nilikuwa nikiagana nae mara baada ya maongezi.Kushikana nae mkono hivi na Nabii huyu Tito haimaanishi kuwa nilimsapoti au kumpinga kwa mahubiri yake bali nilimsikiliza tu..Swali la kwanza nililomuuliza ni ;=The great:Inasemekana wewe ni nabii wa uongo?.Nabii Tito:.Ni uongo gani ninaosema wakati kila kitu kimeandikwa katika biblia takatifu?kunywa pombe si dhambi,kwenda disco si dhambi,Dhambi ya ZINAA kwa mwanaume haimuhusu ndio maana mwanaume hana talaka,Kutumia CONDOM ni dhambi kubwa sana maana tendo la ndoa si starehe bali ni uumbaji(creation)hivyo unapotumia condom na kutupa inamaana unaua viumbe aliokupa MUNGU.

Hapo nabii Tito akisema kuwa kuwa na wanawake wengi si dhambi Mungu anapenda hivyo akatolea mfano katika biblia wa mfalme Suleiman aliyekuwa na wanawake wengi sana lakini bado alikuwa ni kipenzi cha MUNGU.Yeye nabii TITO akasema mwenyewe ana wake wa3.wawili wako hapa DAR,mmoja yuko ARUSHA..na ana mpango wa kuongeza wake mpaka wafike saba na taarifa hizi kashawaambia wake zake,Nabii Tito ana watoto 7 wake kabisa hivyo kuendelea kushikilia msimamo wake wa suala hili katika imani yake.

huu ni msalaba anaouvaa shingoni.

karatasi zake anazoziuza shilingi elfu moja..baadhi ya mambo anayozungumzia ni ;=kunywa pombe na kula nguruwe si dhambi,kuoa wanawake wengi na kutoa talaka si dhambi kabisa,mwanaume dhambi ya zinaa haimuhusu kabisa,wababa ni dhambi kutumia condom,ni dhambi mwanamke kusalisha na kumtawala mwanaume..katika vipengele vyote hivi katoa na nukuu ya mistari katika biblia,MUNGU ni binadamu tena mwanaume.

mfano wa karatasi zake

maneno yake wakati fulani ni comedy tupu

The great nikimtafakari huyu Nabii TITO,HII DUNIA,MUNGU WETU NA NA MAKANISA YETU YA KIROHO,NA BAADHI YA WAANDISHI WA VITABU MBALIMBALI KAMA:=DA VINCH CODE..yeye anasema YESU alioa.KARL MAX..haamini kama Mungu yupo tena anakipinga kifo akisema 'death is a mistake'.ALEXANDER THE GREAT ANASEMA:=Jesus story is just a myth story....JAMANI TUNAENDA WAPI NA HII DUNIA KWA SASA????

9 comments:

Kokusima said...

Ee Mungu tusaidie, huu ndiyo mwisho wa dunia kweli. Yani unaona anayofundisha ni madhambi madhambi madhambi makubwa, tena anajifanya nabii, yani huyu ni nabii wa uhongo kabisa bila hata kuanza kujadiliana. Mungu atuepushie huyu ibilisi mapema.

tunaenda wapi dunia hii jamani?? Tushike imani zetu huu ndiyo mwisho wa dunia Bwaya Yesu aliousema.


Kokusima

Anonymous said...

nafikiri ni wakati muafaka wa serikali na taasisi za kidini kujadili kwa pamoj juu ya huu uhuru wa kuabudu, maana huyu jamaa ni mpotoshaji mkubwa,sijui lengo lake ni nini hasa. huyo ni DEVIL'S AGENT.

Peter said...

Mshikaji hebu fanya mazoezi.. kitambi noma we superstar bwana... humuoni mwenzio Ramsey kapungua saivi.. unene sio tija..

Anonymous said...

jamani huyu ni pepo kashuka duniani! mungu atusaidie, ama hakika sitaki hata kumuona live!! asiwazoee watu, anataka kuwateka hawa mastar wetu, mara kaenda kwa JD, REY, sasa kwa KANUMBA! SHINDWA KWA JINA LA YESU

Anonymous said...

Eheeee!!! Umetabiriwa na nabii huyo!! Basi wewe utaanza kutafutwa kama yeye maana yeye hutafutwa na Mungu amuangamize kwa nabii zake za uongo anazozieneza kote. Huyo atapigwa vibaya!! Umefanya vizuri kumuhakikishia kuwa yeye ni nabii wa uongo.Eti kuoa wake wengi!! yeyoyte anayeoa wake wengi, anakuwa amejawa na tamaa, na anatumikia miungu sio Mungu hai.
Amelaaniwa Tito, asipotubu na kuachana na wake wengi , na kumrudia Mungu, huyo ataangamia.

Anonymous said...

hahahaaaaaaa
Kweli kazi ipo

Kila mtu ashike imani yake,hawa ni manabii wa uwongo tuu!!!

Lil-Holland

Albert said...

Eeh Bwana Kaka Kanumba, huu jamaa msipokua makini atawapotosha na kuwaangamiza. Ni kwa nini hasa viongozi wa nchi na wananchi pia msimfukuze au kumshika mumweke jera? Huu Tito ataleta balaa kwa Tanzania kwani anamkufuru MUNGU wa kweli yule anaesemwa kwenye wimbo wa Taifa.
Nawaombeni mshughulikieni!
Albert
Perth, Western Australia

Anonymous said...

mama yangu!hata ukimcheki huyo nabii kavaa mcheni kama wa 50cents yani unakua na nakshi kama diamonds nadhani ni moja kati ya mapepo mabaya yanayo anza yani up coming demons,usiende tena kanumba hilo ni pepo!yani pombe na kuoa wake wengi ruksa?JUSUS!!ASHINDWEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Huyu jamaa anataka kupata waumini na wamuongezee sadaka nyingi kanisani kwake. Maana aamesoma na kujua matatizo yote yanayowakela watu wote kwa madhehebu yote.

Kuoa wake wengi wakristo
kula ngurue waisilamu
pombe warokole
Taraka wakristo
Ujanja mwingi mjini hapa....