Star Times

Star Times

Mercy Beauty Parlour

Mercy Beauty Parlour

May 4, 2010

SERIKALI YATOA KIJIJI CHA VISEGESE-KISARAWE KWA WASANII WOTE KUWEKA MAKAZI YAO HAPO

Jana nilipata nafasi ya kujumuika na wasanii wenzangu toka fani mbalimbali kama uigizaji,mziki,uchoraji,sarakasi,mitindo,uchongaji nk kutembelea kijiji cha visegese maeneo ya kisarawe ambapo serikali kupitia shirikisho la wasanii Tanzania(shiwata)tumepewa nafasi yetu kuweka makazi yetu hapo hivyo ni haki ya kila msanii kuchukua nafasi hapo kama Marekani wana Hollywood,Nigeria wana Nollywood,sisi je?tujitokeze kwa wingi jamani tukiendekeze hicho kijiji maana ni chetu ila cha kushangaza respond ya wasanii imekuwa ndogo sasa sijui na hapo tumlaumu nani?ni rahisi fika ofisi za shiwata hapo chuo cha splended ilala muulizie teacher utapewa maelezo namna ya kujiunga maana ni lazima kwanza uwe mwanachama wa shiwata mwenye kitambulisho na uliyelipa ada yako ya kila mwaka,mimi The great ni mwanachama hai wa shiwata na nimeshatembelea hicho kijiji,hatua zote nimezimaliza kwa sasa nasubiria tu kupewa ki sehemu changu...wasanii wenzangu ebu jitokezeni jamani MSIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO. msafara wa kuanza kukikagua kijiji ulianza hivi,the great nami nikiwepo

sehemu zingine ilibidi kuvua viatu ili kufika ilipo sehemu yetu,nyuma yangu ni teacher wa splended na ndiye mwenyekiti wa shiwata

hii ni sehemu tu ya ardhi ya kijiji hicho tulichopewa wasanii

baadhi ya wasanii wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kufika katika mpaka wetu wa kijiji hicho mwenye kofia kubwa ni mwanamziki mkongwe King kiki.

baadhi ya wanakijiji waliotupokea pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kwa pamoja katika picha

2 comments:

Anonymous said...

Kwanza nakupongeza kanumba kwa juhudi zako,
yaani wewe unataka maendeleo makubwa ya filamu hapa Bongo,na naamini utafika mbali sana kaka yake.
Unajua serikali imefanya kitu kizuri sana na sasa wasiseme kuwa wasanii hawana mahali pa kufanyia shughuli,
Kwenye hicho kijijini watu wanaweza kuanza kujenga nyumba za majani kuact kama kijijini na kidogo kidogo mkipata mkopo mnaweza kuanza kujenga nyumba za kuactia ambazo zinaweza kubadilishwa decoration kutokana na movie yenyewe inasemaje,ni kitu ambacho kinawezekana kama mkishirikiana,
na hii sio rahisi kufanya msanii mwenyewe hadi wote mshirikiane ndio panawezekana,
kumbuka Umoja ni Nguvu na utenganp ni dhaifu.
Mimi naammini kabisa kutopuuzia kwako tena kama wewe Msanii mkubwa sana kwa hapa tanzania they like it or not wewe uko juu zaidi ya wote na umeweza kuitikia wito huo basi utavuta na wengine wengi,
Show them the way bro yake na you will stay on Top forever,
kwa kuuza kwao surabila manufaa na kutoangalia mbele kunani ndio kunawafanya wabaki chini siku zote.
watakuwa wanakuona tu wewe mara leo Nigeria,kesho South Afrika ,na keshom kutwa hollywood au bollywood

Anonymous said...

Kwanza hongera mdogo wangu nyota yako iko juu wewe ni not only the great but the greatest bwana kweli unafanya makamuzi yaukweli yenye akili pili nimefurahi kuona unafanya tena movie na wema sepetu kwamba mbali yakashikashi na magazeti lakini umekuwa msanii waukweli kucheza nae movie ina maana mko kazini uleti zakiswazi sijui tuna bifu hapana, wewe ni mkristu na jasiri hongera bwana mdogo ndo maana unaona mbele kwaroho yako hiyo utafika mbali, ila la msingi picha za bloguni zimepauka bwana cjui ni camera au ninini? Lifanyie kazi